Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Video: Marekani yaanza mashambulizi ya anga Syria kuilenga ISI Majeshi ya Marekani yameanza rasmi mashambulizi ya anga nchini Syria yakilenga kundi la kigaidi la ISIS (Islamic State of Iraq and Syria).
Makao Makuu ya Ulinzi ya Marekani yameeleza kuwa wanafanya mashambulizi ya mchanganyiko kwa kutumia mabomu, wapiganaji wa ardhini pamoja na majeshi ya Anga kutoka nchi za Mashariki ya Kati zinazowaunga mkono.
Lakini habari za mashambulizi yaliyoanza zilitolewa na raia wa Syria aliyetweet kuhusu kile anachokisikia katika mji aliopo wa Raqqa ambako kuna makao makuu ya kundi hilo.
Mtu huyo anaetumia jina la Abdulkader Hariri aliandika kuwa milipuko mikubwa imelenga makao makuu ya ISIS na kwamba anga lote limejaa ndege za kivita na drones.
Baadae Agency ya wanaharakati nchini Syria ilipost video fupi inayoonesha kwa mbali mashambulizi ya Marekani.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top