Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Taarifa zilizopatikana hivi punde zinaeleza kwamba kikundi cha kigaidi cha Dola ya Kiislamu (IS) kimemchinja kwa kumkata kichwa, David Haines, Mwingereza mfanyakazi wa shirika la misaada, kwa mujibu wa video iliyosambazwa na kikundi hicho.
 
Video ya mauaji hayo ya kinyama inaanza kwa kuonyesha hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuhusu Iraki, ikifuatiwa na ujumbe kwa washirika wa Marekani dhidi ya kikundi hicho, na inahitimishwa kwa tukio la kuogofya la kukatwa kichwa kwa Davidi ambaye ni Mskochi.
 
Tukio hilo limetokea na kurekodiwa katikati ya jangwa. Baada ya hotuba ya Cameron, mtu aliyejifunga kitambaa kuficha uso huku ameshikilia kisu anaonekana amesimama mbele ya David ambaye amepiga magoti, na kuamriwa kusoma 'hotuba ya mwisho.'
 
Katika hotuba hiyo fupi, Mwingereza huyo anasema, namnukuu,"Ninapenda kubainisha kuwa ninakulaumu Davdi Cameron kwa kuuawa kwangu.Umeingia kwa hiari katika ushirika na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislam, kama alivyofanya mtangulizi wako Tony Blair."
 
Baada ya kusoma taarifa hiyo, Davidi anakatwa kichwa kisha Mwingereza mwingine, Alan Henning anaonyeshwa akitishiwa maisha. 
  
Mtu aliyefanya uchinjaji huo anaonekana kuwa ni yuleyule aliyewachinja watu wengine wawili kabla ya tukio hili. 
  
Kadhalika, anasikika akitoa onyo, namnukuu, "Iwapo wewe Cameron utaendelea kupambana na Dola ya Kiislam, basi wewe, kama bwana wako Obama, mikono yenu itakuwa na damu ya watu walio mateka wetu."
Tazama  Video  hapo  chini( Video Inatisha)  

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top