Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
  Kanye West agoma kuendelea na show hadi walemavu wa miguu wasimame, amtuma bodyguard kuhakikisha  Kanye West alikuwa kwenye tamasha lake nchini Australia wakati huu na aliamua kuweka msimamo kwa maneno aliyoyasema kuwataka mashabiki wote kusimama na kucheza wakati anaimba la sivyo asingeendelea na show.

“'I can't do this song, I can't do this show until everybody stand up. Unless you got a handicap pass  and you get special parking and s**t.'Imma see you if you ain't standing up, believe me, I'm very good at that.”. Alisema.
Kwa bahati mbaya zoezi hilo lilikuwa gumu kwa mashabiki wawili waliokuwa wamekaa kwenye kiti maalum cha kuwasaidia kutembea na huenda walikuwa walemavu ama wagonjwa wa miguu.

Kanye alisimamisha zoezi la kuimba ingawa watu waliendelea kumpigia kelele wakimuonesha ishara kuwa watu hao walikuwa kwenye wheelchairs.
Rapper huyo hakuamini maneno tu na alimtuma mlinzi wake aitwae Pascal kuhakikisha na kumletea majibu.
Pascal aliporudi alimhakikishia kuwa kweli walikuwa kwenye wheelchairs na ndipo alipolegeza masharti na kuendelea na show.
“He is in a wheelchair? It’s fine!” Alisikika Kanye West.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top