March 30, 2025 05:01:39 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


India imewakilisha 'Mangalyaan katika sayari ya Mars

Wanasayansi wa anga za juu nchini India wanasema kuwa chombo chao cha safari za anga za juu kwa sasa kinazunguka sayari ya Mars.
Hii ndiyo mara ya kwanza kwa India kutuma mtambo wake kwenda kwa sayari hiyo, safari ambayo imepata umaarufu kutokana na gharama yake ya chini kabisa ya dola milioni 75 pekee.

India ndilo taifa la nne duniani kufaulu kufikisha chombo katika sayari ya Mars.
Mataifa mengine ambayo yamewasilisha vyombo vya utafiti wa anga za juu katika sayari hiyo ni Marekani Urusi na muungano wa mataifa ya Ulaya.

Chombo hicho ''The Mangalyaan robotic probe'' kinatarajiwa kuanza upekuzi na uchunguzi wa hali ya anga katika sayari hiyo nyekundu.
Waziri muu nchini India Narendra Modi ambaye alishuduia mafaniko ya chombo hicho kilichoanza safari yake miezi kumi iliyopita aliwapongeza wanaayansi hao kwa ufanisi huo mkubwa.

Roketi ya India 'Mangalyaan iliyotua katika sayari ya Mars

Aliwaambia kuwa mafanikio ya safari za anga za ju nchini India ni mfano mwema wa hatua ambazo taifa hilo linaweza kupiga akisema kuwa ana mpango wa kuboresha kitengo hicho.
Shirikisho la anga za mbali la Marekani NASA ambalo lilifikisha chombo chake ''Maven'' katika sayari ya Mars Jumatatu wiki hii, liliwapongeza wanasayansi wa India kwa ufanisi wao.
Kupitia kwa ujumbe wa mtandao wa Twitter NASA iliandika kuwa ''Tunawapongeza @ISRO kwa kuwasili katika sayari ya Mars. Mtajiunga na @MarsOrbiter kutathmini hali ilivyo katika sayari hiyo".
CREDIT: BBC

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
25 Sep 2014

Post a Comment

 
Top