NYOTA wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki wa Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa ‘kihasarahasara’.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’akiwa na mrembo huyo.
Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20, 2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya Yanga na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji walishinda 2-0. Steve alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani (zinazotumiwa na Yanga).
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo walipozomewa na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa kuwa, demu huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara hadharani.
Mrembo huyo akikatiza mbembezoni mwa uwanja.
Baadaye mwandishi wetu alimfuta Steve na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Wale kunizomea ni haki yao ila mimi na mwenzangu tumeona kama wametushangilia.”
Alipoulizwa uhusiano wake na demu huyo,Steve aligoma kujibu badala yake alikimbilia kwa mwandishi mwingine wa Global Publishers (Musa Mateja) na kuomba msaada. Mrembo huyo alipotakiwa kuzungumzia tukio hilola kuzomewa na sababu za yeye kuvaa vile, alijibu kwa mkato: “Kuzomea ni haki yao, mimi nawaona kama washamba tu.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Bodi ya Mikopo yatangaza majina 1,091 ya wadaiwa Ambao Hawataki Kulipa (Awamu ya kwanza).....Bonyeza Hapa Ujitazame Kama na Wewe Jina Lako Lipo28 Jul 20160
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), inawaarifu wadaiwa wote ambao mpaka hivi sa...Read more ?
- Picha:Uzinduzi Wa Kitabu Cha Kanumba Hapo Jana12 Jan 20150
NAIBU Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga, jana amezindua rasmi kitab...Read more ?
- Odama: Ndoa Haitanifanya Niache Filamu08 Jan 20150
Na Laurent Samatta MCHEZA filamu za Kibongo Jennifer Kyaka ‘Odama’, amedai kuwa mwanaume a...Read more ?
- Baby Madaha: Nikifa Nisizikwa Katika Makaburi ya Kinondoni06 Jan 20150
WAKATI baadhi ya wasanii wa hapa jijini, Dar wakifa huzikwa hapahapa, jambo hilo limekuwa ni ...Read more ?
- MCHUMBA: MASOGANGE KANISALITI22 Nov 20140
STORI: Musa MatejaMCHUMBA wa Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ aitwaye Evance K...Read more ?
- KAJALA MASANJA ATAMANI KUPATA MTOTO WA PILI22 Nov 20140
MWIGIZAJI Kajala Masanja amefunguka kuwa anatamani kuongeza mtoto wa pili kwani tayari aliyenaye am...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment