March 17, 2025 11:50:56 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Like
Wakati flani katika maisha sisi wanasanaa na waandishi wa habari tunahitilifiana kwa kutokuheshimiana tu; na kwa hakika kama tungetanguliza heshima miongoni mwetu daima tusingekwaruzana hata kidogo ukizingatia kuwa tasnia zetu zinategemeana sana,hebu angalia muandishi kama huyu anatumia picha yangu mimi na dada asiemjua halafu bila kuniuliza mimi kama muhusika kuwa huyo dada ninani na anauhusiano gani namimi yeye muandishi moja kwa moja anapeleka picha kwenye mitandao/magazeti na bila aibu,woga na kuheshimu tasnia yake anaandika kuwa'siku moja baada ya 40 ya mkewe afande anamwanamke mpya' wakati si kweli,NIMEFAIDHAIKA SANA!, 
ukiachilia mbali suala la kunidhalilisha katika jamii au kunitia ubaya mbele za watu kwa kunisingizia kuwa nimekutwa na mwanamke siku moja baada ya arobaini ya mzazi mwenzangu bado pia sijui hasa huyu muandishi dhamira yake kuu ya kutumia picha hiyo ya kawaida na kuitungia habari ya uongo kama hiyo ilikuwa nini?au ndio tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu?chondechonde ndugu wanahabari kalam zenu mkizitumia vibaya huwa ni silaha nzito kuliko ndege za kivita za jesh la marekani,kwa imani ya dini yangu hata kabla ya kifo cha mzazi mwenzangu ningeweza kuruhusiwa kufunga ndoa na bint mwingine hasa ukizingatia mimi na mama wa hasa ukizingatia kuwa mimi na mama watoto wangu tulikuwa tumeshatengana mwaka mmoja kabla hajafikwa na umauti, lakini kwangu mimi bado sikuwa na sina wazo hilo la kuoa mpaka sasa ingawa kama mwanaume"rijali" ninae rafiki mwema na wakawaida tu ambae kimsingi tunaheshimiana sana,

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
25 Sep 2014

Post a Comment

 
Top