Mashua iliyobeba wakimbizi kama 170 ikielekea Ulaya, imezama mwambao wa Libya na inahofiwa watu wengi wamekufa.
Jeshi la wanamaji la Libya limewaokoa watu 17 na inawasaka abiria wengine.
Wavuvi waliwazindua wakuu ambao walituma waokozi.Mashua hiyo ilikuwa na shida punde baada ya kuondoka bandari ya Qarabouli, mashariki ya mji mkuu, Tripoli.
Lakini afisa wa walinzi wa pwani wa Libya alisema kikosi chake hakina zana za kutosha, na mara nyingi wanahitaji kuazima mashua kufanya kazi hizo ya uokozi.
Na ndege imeshambulia maeneo ya wapiganaji Waislamu karibu na uwanja wa ndege wa Tripoli na kuuwa watu 10.
Ndege hiyo ililenga kambi ya jeshi kusini ya Tripoli, ambayo zamani ilikuwa makao makuu ya Muammar Gaddafi.
Hiyo ni mara ya pili kwa ndege kushambulia eneo hilo katika juma moja.
Jenerali anayepinga wapiganaji hao, Khalifa Haftar, alisema watu wake ndio waliofanya shambulio la mwanzo lakini wadadisi wanashuku kama ana uwezo huo.
Kikosi kimoja cha jeshi la wanahewa kimelaumu ndege kutoka nchi za nje.
>>>>>>BBC
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment