Arsenal, wakiwa Ugenini huko Goodison Park, walitoka nyuma kwa Bao 2-0 na kupata Sare ya Bao 2-2 walipocheza na Everton huku Bao lao la Pili likifungwa mwishoni katika dakika za Majeruhi.
Huku wakikumbuka kichapo cha hapo hapo Goodison Park Mwezi Aprili walipopigwa Bao 3-0 na Everton, Arsenal walijikuta wako Bao 2-0 nyuma hadi Mapumziko.
Bao la kwanza la Everton lilifungwa na Fulbeki Seamus Coleman kwa kichwa katika Dakika ya 19 baada ya kazi safi ya Gareth Barry.
Bao la pili kwa Everton lilipatikana Dakika ya 45 baada Romelu Lukaku kuwachambua Mabeki wa Arsenal, Per Mertesacker na Monreal, na kumpasia Steven Naismith aliepiga Shuti la chini na kumpita Kipa Wojciech Szczesny.
Arsenal walianza Kipindi cha Pili kwa kumwingiza Olivier Groud badala ya Mchezaji wao mpya Alexis Sanchez ambae katika Kipindi cha Kwanza chote, akicheza kama Sentafowadi, alishindwa kuingia kwenye boksi hata mara moja.
Kipindi cha Pili, Arsenal walijitutumua lakini Everton walijizatiti sana kulinda Bao zao lakini baada ya Arsenal kufanya mabadiliko kwa kuwaingiza Santi Cazorla na Joel Campbell badala ya Wilshere na Oxlade-Chamberlain kidogo uhai ulipatikana.
Arsenal wakafunga Bao lao la kwanza Dakika ya 83 kupitia Aaron Ramsey kufuatia kazi nzuri ya Santi Cazorla na kusawazisha katika Dakika za Majeruhi kwa Bao la Olivier Giroud.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment