Malaysia iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa baada ya kupokea miili 20 ya wahanga wa mkasa wa ndege ya Malaysia MH17 iliyotunguliwa Ukraine mwezi uliopita.
Miili ilipokelewa na kupewa heshima za kitaifa.
Majeneza yalikuwa yamefunikwa na bendera za taifa na ilibebwa na wanajeshi kabla ya kusafirishwa kwa magari ya kubeba maiti iliyozipitishwa karibu na mfalme na waziri mkuu kabla ya kukabidhiwa kwa familia husika.
MH17 iliangushwa katika eneo la waasi Mashariki ya Ukraine mwezi uliopita.
Machi mwaka huu ndege nyingine ya Malaysia ilitoweka katika bahari hindi amesema kuwa shirika hilo la ndege linaendelea kutatizwa na matukio hayo mawili.
Wasafiri wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo ya MH17 walifariki 43 kati yao wakiwa raiya wa Malaysia.
Ndege iliyobeba miili hiyo ilikuwa imetengwa kwaajili ya shughuli hiyo kutoka Amsterdam na kutua saa nne saa za huko.
Bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kote nchini na dakika moja ya kimya itazingatiwa.
Kikundi kidogo cha wanajeshi wa Malaysia kilienda hadi karibu na ndege hiyo kulinda majeneza hayo yalipokuwa yakitolewa kwa ndege huku magari makubwa meupe ya mazishi yakiwa yamepangwa kuzipokea miili hiyo.
Majeneza yote yamefunikwa kwa bendera ya taifa na miili mitatu ya hiyo 20 imechomwa nchini Uholanzi.
New Straits Times ilisema sekta ya uchukuzi ya umma nchini humo ikiwemo ile ya reli ya taifa na reli moja ya Kuala lumpur zitasimamisha shughuli zao kuzingatia dakika mbili za kimya kwa heshima ya wahanga wa mkasa huo.
Vibanda maalum kwenye barabara kuu vitakuwa na ishara za kielektroniki kuwaeleza madereva washuke kutoka kwa magari yao ilikutoa heshima.
Msemaji wa ndege za Malaysia alisema kwamba kampuni hiyo ingepanga kipindi cha maombi ambacho kingefanywa wazi kwa mtu yeyote ili kutoa maombi na heshima zao kwa walioaga.
Akiongeza alisema kwamba kampuni hiyo ya ndege za Malaysia imehuzunishwa sana na tukio hilo la kuogofya .
Aidha imekuwa muda mrefu wa kungoja kwa familia na marafiki wa wasafiri na wafanyakazi waliokuwa katika ndege MH17.
Hii ni mara ya kwanza Malaysia inaendeleza siku ya maombolezi ya taifa kwa wananchi wa kawaida.
Heshima hiyo kitamaduni imekuwa ikipewa familia ya mfalme na wakuu serikalini.
Kufikia sasa waathiriwa 28 wa Malaysia wametambuliwa nchini Uholanzi ambako utafiti wa kimataifa kuhusiana na kuanguka kwa ndege hiyo mashariki mwa Ukraine unaendelezwa.
Zaidi ya majeneza 200 iliyo na mabaki ya waathiriwa kufikia sasa yamepelekwa Uholanzi lakini uchunguzi unazuiliwa na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali ya Ukraine na waasi yanayoiunga mkono Urusi karibu na eneo ambalo ndege hiyo ilianguka.
CHANZO BBS SWAHILI
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment