Bomu lililotegwa kwenye gari
limelipuka na kuua watu wanne karibu na Bunge la Somalia na wengine
kujeruhiwa, maafisa wa Polisi wamesema.
Kabla ya hapo, mshambuliaji huyo alijaribu kuingia katika wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, lakini alizuiliwa.
Wapiganaji hao Waislamu wamelaumiwa kwa shambulio hilo. Al-Shabaab ilisema itazidisha mashambulio wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mlipuko mwingine uliofanywa na waasi hao katika majengo ya bunge mwezi Mei uliua watu 10.
Kundi la Al shabaab lilipoteza udhibithi katika mji mkuu wa Mogadishu tangu mwaka 2011 na tangu wakati huo limekuwa likiendesha mashambulizi ya mabomu na kufanya mauaji.
Mapema wiki hii Mbunge maarufu Ahmed Mohamud Hayd, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji huo, katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab.
Chanzo bbcswahili
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment