Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
SIKU chache
zimekatika tangu kusambazwa kwa picha feki inayodaiwa ni ya mama wa
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu, wawili hao wako kwenye
mkakati mzito wa kuwasomea kisomo cha Albadili wale wote waliohusika kwa
namna yoyote ile kuitengeneza picha hiyo na kuitupia mitandaoni.
Picha
hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na kichwa
cha mama Wema, lakini sehemu ya kuanzia shingoni kwenda chini si yeye
na mhusika alikuwa hana nguo, ilizua gumzo kwa wiki mbili sasa huku watu
wanaojiita Timu Dengue wakitajwa kuhusika.
KINYWANI MWA CHANZO CHA HABARI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Wema na mwanaye wameamua kusoma
Albadili ili kuwaadabisha wale wote waliohusika na sakata hilo lenye
kufedhehesha.
“Mama Wema na mwanaye walikasirishwa sana na watu waliotengeneza ile
picha na kuitupia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.
“Wiki
iliyopita baadhi ya wasamaria wema walikwenda nyumbani kwa mama Wema na
kumtajia majina ya wahusika, lakini hawakuwa na ushahidi hivyo yeye na
Wema wameamua kujiunga kiimani zaidi kwa kusoma Albadili.
“Wamesema
kwanza kabla ya tukio hilo la Abdadili wametoa siku saba kwa yeyote
anayejijua amehusika na picha zile za kutengeneza aende mwenyewe kwa
mama Wema, nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar) ili kuomba msamaha.
“Kama
zitapita siku saba na hakuna atakayejitokeza, Albadili itasomwa na mmoja
baada ya mwingine watakufa. Tayari wameshawasiliana na mashehe ambao
watasoma Albadili hiyo,” kilisema chanzo hicho.
WEMA AYEYUKA HEWANI
Baada ya kusikia kutoka kwa chanzo chetu cha uhakika, juzi paparazi
lilimsaka Wema ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai hayo
lakini muda mwingi wa maandalizi ya habari hii, simu yake haikuwa
hewani!
MAMA WEMA SASA
Baada ya kumkosa Wema, paparazi lilimtafuta mama yake, naye kwa njia
ya simu na alipopatikana aliombwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo.
KUHUSU ALBADILIAkizungumza kwa hasira huku sauti yake ikionesha dalili kwamba bado hayuko sawa, mama Wema alisema:
“Ni
kweli, nimeshapanga kufanya hivyo, nitasoma Albadili. Haiwezekani watu
wakae na kuamua kunichafua mimi, nimewakosea nini cha mno mpaka kufikia
kufanya vile! Siwezi kukubali hata kidogo.”
KUHUSU MASHEHE
“Ni kweli pia, nimeshawasiliana na mashehe. Wao wako tayari
wanachosubiri ni kupita kwa siku ambazo nimetoa. Kama hakuna
atakayejitokeza kuomba radhi, kisomo cha Albadili kitasomwa, wataanza
kupukutika mmoja baada ya mwingine kweli nasema.”
SIKU SABA ZINAANZA LINI?
“Jumamosi ijayo (leo) itakuwa siku ya kwanza. Kwa hiyo mpaka Ijumaa ya Julai 11 (mwaka huu), itakuwa siku ya mwisho.”
NENO LAKE KWA WAHUSIKA
“Nawaambia wale wote wanaojijua walihusika na ile picha ya uongo, ya
kutumbukiza kichwa changu kwenye picha nyingine na wale waliohusika
kuitupia kwenye mitandao, waje waniombe radhi kabla siku saba
hazijaisha, sitanii jamani.”
UKWELI WAKE
“Mimi ni Muislamu safi, nasema sijawahi kupiga picha za namna hiyo
katika maisha yangu tangu nizaliwe mpaka utu uzima wangu huu na wala
sijawahi kufikiria.”
KUMBUKUMBU YA WEMA
Wema azimia!
Habari ile ilimhusu Wema kupoteza fahamu kufuatia kuiona picha hiyo kwenye mitandao akidai ililenga kumchafulia mama yake jina.
KILIO KWA TCRA
Kumekuwa na wimbi la watu kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii
ambapo ukiacha watu maarufu kutengenezewa picha chafu, pia wanafunzi wa
vyuo wamekuwa waathirika wakubwa.
Hata
hivyo, baadhi ya wananchi waliowahi kuzungumza na gazeti hili kwa
nyakati tofauti walitoa kilio chao kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudhibiti usambazwaji wa
picha chafu mitandaoni.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment