Majeshi
Maalum (Special Forces) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda
amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni
mwa vikosi bora 35 vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa
na ufanisi wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa
vizuri.Kwa mujibu wa Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania
na jeshi lake ni nchi pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake
miongoni mwa majeshi bora duniani.Chini ya kichwa cha habari “35 Most
Badass Elite Fighting Units from Around the World” mwandishi, Micky Wren
anaandika kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani, yamefundishwa kwa
kiwango cha juu kabisa, yana silaha za kisasa kabisa, yameandaliwa
vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi na yenye uwezo
kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia kumaliza uhuni wa
utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo mkubwa.
Mwandishi anasema kuwa orodha hiyo haikupangwa kwa mtitiriko wa uwezo wa kijeshi wa kila kikundi.
Vikosi vilivyoko kwenye orodha hiyo ni kile cha Seal cha Jeshi la Maji
la Marekani, SAS cha Jeshi la Uingereza, Huntsmen Corps cha Majeshi
Maalum ya Denmark, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Kikosi cha MARSOC,
Majeshi Maalum ya Taiwan ambayo yanatumia kinga za usoni zisizoweza
kuingiliwa na risasi na Kikosi cha Irish Army Rangers cha Jamhuri ya
Ireland.
Vingine ni Gendarmerie cha Serbia, Kikosi Maalum cha Kukabiliana na
Ugaidi cha JTF2 cha Canada, Majeshi Maalum ya Uholanzi, Kikosi cha SBS,
Majeshi Maalum ya Jamhuri ya Korea, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Majeshi
Maalum ya Ubelgiji, Kikosi cha MJK cha Norway, Canadian Joint Response
Unit cha Canada, Majeshi Maalum ya Norway, Kikosi cha French Commando
Marine, Majeshi Maalum ya New Zealand, Kikosi cha Norwegian Armed Forces
Special Command na Kikosi cha Polish Grom cha Poland.
Vingine ni Kikosi cha US Army Special Forces Sniper with Remington
Modular Sniper Rifle, Majeshi Maalum ya Marekani, Majeshi Maalum ya
Indonesia, Majeshi Maalum ya Romania, Kikosi cha SASR cha Australia,
Kikosi cha KSK cha Ujerumani, Majeshi Maalum ya Ujerumani, Majeshi
Maalum ya Israel – Shayetet 13, Majeshi Maalum ya Urusi – Spetsnaz,
Majeshi Maalum ya Austria – Jagdkommando, Majeshi Maalum ya Iraq,
Majeshi Maalum ya Ujerumani ya SEK-M na Majeshi Maalum ya Peru.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
3 Julai, 2014
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment