Matukio
ya milipuko ya mabomu yameendelea kuuandama mkoa wa Arusha ambapo hapo
jana majira ya saa tano Usiku katika eneo la Majengo ya chini jijijni
Arusha kumetokea mlipuko wa bomu linalosadikiwa kuwa ni la kutengenezwa,
nyumbani kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Answar Suna Youth Center Shekh
Sudi Ali Sudi.
Tukio ambalo limesababisha watu wawili kujeruhiwa vibaya na kusababisha uharibifu wa mali katika nyumba ya mkurugenzi huyo.
Ni
majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu ambalo limetokea jana usiku
nyumbani kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Aswar Suna Youth Center Shekh Sudi
Ali Sudi na Muhad Husen wakizungumza kwa tabu wakati walipokuwa
wakielezea namna tukio hilo lilivyotokea.
Tukio
ambalo limetokea wakati watu hao wakiwa wanajiandaa kula daku, mara
baada ya kuvunjwa kwa kioo cha dirisha, na watu wasiojulikana kisha
kurusha ndani kitu kinachasadikika kuwa bomu na kusababisha mlipuko
mkubwa uliowasababishia majeraha.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea
muda mfupi baada ya taarifa za Shekh huyo ambazo amezitoa kwa jeshi
hilo kuwa lipo kundi la watu ambalo limetishia kumdhuru kutokana na
msimamo wake katika masuala ya imani yake.
Aidha
kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na Mbunge wa
Jimbo hilo Godbless Lema wamesema ipo haja ya viongozi wa dini na
taasisi zake kuangalia namna nzuri ya kumaliza migogoro yao na
kujiepusha na matumizi ya njia zisizokuwa sahihi katika kutatua migogoro
ili kulinda amani ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Tukio
hili la mlipuko wa bomu linatajwa kuwa la tano kutokea jijini Arusha
baada ya tukio la kutupiwa bomu katibu wa BAKWATA Mkoa wa Arusha mwaka
2012 , na kufuatiwa na matukio ya milipuko Katika Parokia ya Yosefu
Mfanyakazi iliyopo Olasiti, Mkutano wa CHADEMA Katika viwanja vya Soweto
na lile la mlipuko katika baa ya Arusha Night park.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment