Mwanamke mmoja
ameripotiwa kumchoma kisu na kumuua mwalimu wa kike wa shule ya msingi
mbele ya wanafunzi wake katika mji wa Albi ulio kusini mwa Ufaransa.
Mwendesha
Mashtaka wa Albi, Claude Derens ameiambia AFP kuwa tukio hilo limetokea
jana (July 4) majira ya asubuhi kwa saa za Ufaransa na kwamba uchunguzi
unafanyika ili kubaini sababu zilizopelekea mwanamke huyo kufanya tukio
hilo la kikatili.
“Mama huyo
alionekana akiwa na kisu na akamchoma mwalimu wa kike mwenye umri wa
miaka 34 mbele ya wanafunzi wake, sababu itafahamika baada ya uchunguzi
kukamilika.” Claude Derens aliiambia AFP.
Aliongeza kuwa
baada ya tukio hilo, rais wa Ufaransa Francois Hollande alimtuma waziri
wa elimu, Benoit Hamon haraka katika shule hiyo ili kuhakikisha
anachukua hatua kama mwakilishi wa serikali.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment