Marehemu mzee Halfan Mohammed Mtonga enzi za uhai wake
Stori ya
kifo cha mzee Halfan Mohammed Mtonga (82) mkazi wa Kijiji cha Pera,
Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani hapa kinachodaiwa kutokana na
kuvunjwa shingo, inasikitisha.Tukio hilo lilitokea Julai 3, mwaka huu
nyumbani kwake baada ya kuzidiwa, hali yake ilipobadilika siku kadhaa
tangu aliporuhusiwa hospitalini.
Marehemu mzee Halfan Mohammed Mtonga (82) mkazi wa Kijiji cha Pela, Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani akisindikizwa katika safari yake ya mwisho.
Akisimulia
tukio zima kwa majonzi, mjane wa marehemu Aisha Amir (75) alisema,
ameumia sana kumpoteza mume wake kipenzi ambaye anadai kukatishwa uhai
na mpwa wake aliyemtaja kwa jina moja la Sabata aliyemshambulia na
kumvunja shingo.
“Siku
ya tukio tulikuwa tumelala mimi na mume wangu, ghafla tukaona mwanga wa
tochi, tulipofuatilia tukagundua ni Sabata, nilipomwambia anataka nini,
akatishia kuniua. Alisema nikae kimya.
“Alimwamrisha marehemu aamke ili ampe chipsi na soda alizomletea
lakini alikataa kutokana na hali yake kiafya kuwa mbaya. Alipoona
amekataa, alimsukuma chini kwa nguvu, mzee akaanza kulia akilalamikia
maumivu makali ya shingo. Tukiwa tumeduwaa, Sabata alianza kumwagia haja
ndogo usoni,” alisema Bi. Aisha akimwaga machozi.
Alisema
baada ya tukio hilo, majirani waliitana kisha kumkimbiza hospitalini kwa
matibabu ambapo uchunguzi ulionyesha kuwa alivunjika shingo.
“Hata
hivyo alifanyiwa matibabu na kuruhusiwa, akaonekana kuwa na hali ya
kuridhisha kabisa, hadi hali yake ilipobadilika nyumbani na kufariki,”
alisema Bi. Aisha.
Naye mtoto wa marehemu, Seleman Halfan alisema muda mfupi kabla ya
baba yake kufariki, alikuwa akilalamika kuuawa na mpwa wake Sabata.
“Mzee
wangu amekufa kifo kibaya sana, sijui ni kwa nini huyo Sabata alifikia
hatua hiyo. Kila wakati alikuwa anasema; Sabata unaniua, Sabata unaniua!
Yaani ametuacha na maswali mengi sana. Lakini tunaamini sheria itafuata
mkondo wake,” alisema Seleman.
Mtuhumiwa
huyo alikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Chalinze kisha
kupelekwa mahabusu katika Gereza la Mifugo la Ubena, Chalinze mkoani
hapa akisubiri hatua zaidi za kisheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Nesphory Matei alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa
vyombo vya dola dhidi ya watu wasio wema kwenye jamii.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment