Swala la kubadili rangi ya ngozi limekuwa kama msumari moto,
kunao wanaoliunga mkono na wale wanaolipinga swala hilo katu hawawezi
kulifanya.
Baadhi wanasema kuwa ni wanawake wasiojithamini na kujiamini
pekee ndio wenye kujichubua ngozi.
Mjadala huo ukiendelea, wasichana wengi wanajitafutia
umaarufu sio Marekani na Uingereza tu bali hata katika kanda ya Afrika ya
Mashariki. Wasichana hao wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kupata huo
umaarufu.
Mmoja wa wasichana hao ni Vera Sidika anayejulikana sana
nchini Kenya na Afrika mashariki kwa kuwa na makalio makubwa ambayo ndiyo
yaliyompa umaarufu wake baada ya kuonekana katika wimbo mmoja wa video uitwao
'You Guy' ambao baadaye ulipigwa marufuku nchini Kenya.
Picha za awali kabla ya Vera kujichubua ngozi
Vera amejizidishia umaarufu kwa kubadili rangi yake ya
ngozi, zamani kidogo akiwa mweusi na sasa amejichubua na kuwa mweupe na pia
kuwaambia watu kuwa kubadili rangi ya ngozi yake ni yeye mwenyewe kujitakia. Hiyo
isiwashughulishe watu.
Vera anajulikana kwa kuwa na mazoea ya kujipiga picha hasa
za makalio yake na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. Vara analinganishwa
sana na Kim Kardhashian hasa kwa sababu ya umbo lake.
Kazi ya Vera hasa ni ya uwanamitido lakini mbali na hilo
Vera hulipwa ili kufika kwenye karamu mbali mbali , kwenye disco na katika
hafla mbali mbali za watu mashuhuri. Yeye pia hulipwa kuwa katika kanda za
video za wanamuziki maarufu Afrika Mashariki.
Alifichua kupitia televisheni Ijumaa kuwa alitumia maelfu ya
dola kubadili rangi ya ngozi yake na kujifanya mweupe.
Shughuli hiyo aliifanyia nchini Uingereza na ilimgharimu
karibu milioni 15 pesa za Kenya, hizo ni dola 170,000 na kwamba tayari kuna
watu wengi wanaotaka sana kujichubua ngozi na kufanana na Vera, kwa mujibu wa
mwanadada huyo.
Vera ni mwanamitindo na anapanga kufungua duka la kuuzwa
bidhaa za urembo
Vera anasema kuwa watu wamemsema sana kwenye mitandao ya kijamii
vibaya kwa sababu
ya anavyoendesha maisha yake. Amewataja kama wanafiki kwa
sababu anasema huku wakiendelea kumsema na kumkosoa kwa kujichubua, wamekuwa
wakimuuliza alichofanya ili na wao watafute pesa wakafanye hivyo kwa wanataka
sana kufanan naye.
Mtindo wa wanawake kujichubua ni swala tata nchini Kenya.
Sio kama India ambako vipodozi vya kujichubua huuzwa wazi wazi. Nchini Kenya
bidhaa hizo, huuzwa kimagendo.
Wataalamu wanasema, wanawake wengi wanaendelea kujichubua
licha ya hatari za bidhaa zinazouzwa kimagendo.
Swala la wanawake kijichubua barani Afrika lilianza
kujadiliwa waziwazi pale ambapo msanii raia wa Cameroon Dencia kuzindua rasmi
bidhaa zake za kuchubua ngozi ziitwazo, Whitenicious.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment