WAKATI mwili wa askari polisi mwenye namba, D 9887 Koplo Joseph
Ngonyani wa Kituo cha Polisi Mkamba, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani
ukisafirishwa leo kwenda mkoani Songea baada ya kuuawa na watu ambao wanadhaniwa kuwa jambazi, majeruhi mmoja kati ya wawili Venance
Francis ambaye ni mgambo, naye amefariki dunia.Francis ambaye naye alijeruhiwa katika tukio hilo baada ya watu hao kuvamia kituo hicho
cha polisi, kupola silaha na risasi, amefariki dunia jana katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, wakati akiendelea
kupatiwa matibabu.Akizungumza na Majira jana, Bi. Annastazia Nyonyani
ambaye marehemu Koplo Nyongani ni baba yake mdogo, alisema mwili huo umesafirishwa jana kwenda Songea, Kijiji cha Namasengo kwa
mazishi."Tumeaga mwili saa sita mchana, saa nane tulianza safari ya
kwenda Kijiji cha Namasengo kwa mazishi ambayo yatafanyika kesho (leo), kwa sasa bado tupo safarini,"alisema.Marehemu Koplo Ngonyani alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa katikaHospitali ya Wilaya ya
Mkuruanga baada ya kukatwa mapanga na watu hao ambao walivamia kituo
hicho na kupora silaha mbili aina ya SMG.Silaha hizo, zote zikiwa na magazini mbili zenye risasi 30 kila mmoja na kuwajeruhi mgambo wawili
waliokuwa kituoni hapo akiwemo marehemu Francis na mwenzake Mariam Mkamba.Akizungumza na Majira, Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaisha, alithibitisha kifo cha marehemu Francis na kuongeza kuwa, mwenzake Mkamba anaendelea na matibabu kwenye Kitengo cha Mifupa (MOI), kilichopo hospitalini hapo."Marehemu alifikishwa hospitalini
hapa juzi akitokea hospitali ya Wilaya ya Mkuranga...amefariki leo
(jana), saa nne asubuhi,"alisema.Taarifa zilizolifikia Majira kutoka
vyanzo mbalimbali, zinasema jeshi hilo linawashikilia baadhi ya watu wakihusishwa na tukio hilo na wanaendelea kuhojiwa.Awali Kamanda wa
Polisi mkoani humo, Ulrich Matei alisema jeshi hilo litahakikisha
silaha zote zilizochukuliwa na watu hao zinapatikana haraka akiwataka wananchi kuwa wavumilivu kuhusiana na tukio hilo.Kamishna Suleiman
KovaKatika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limeunda kikosi maalum cha upelelezi kwa kushirikiana na jeshi hilo mkoani ili kufuatilia tukio la mauaji ya polisi huyo na uporaji
wa silaha.Akizingumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema kikosi hicho kitafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha silaha zilizoporwa zinapatikana na wahusika wanakamatwa.

Credit: Majira
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment