Kijana
mmoja aleyetambulika kwa jina moja la sule amenusurika kifo baada ya
kupingwa na watu wenye asira kali wakimtuhumu kuwa ni mwizi jambo ambalo
baadae lilikuja kubainika kuwa hana hatia yoyote.
Wakizungumza
eneo la feri jijini dar es salaam baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
wamesema kuwa inasikitisha kuona watu wakijichukulia sheria mikononi
bila kuhoji tukio ambapo mara baada ya kipigo ambacho kimemsababishia
majeraha makubwa kijana huyo hakuna mtu aliye jitokeza kulalamika
kuibiwa wala kujulikana kijana huyo ameiba nini.
Akiongea kwa shida kijana huyo amesema kuwa yeye hakuiba chocho na hajui kwa nini watu walimvamia na kuanza kumpiga
Katika
hatua nyingine ya kujaribu kunusuru maisha ya kijana huyo baadhi ya
wasamalia wema waliamua kumfikisha kijana huyo katika vyombo vya usalama
lakini mara baada ya kumfikisha katika kituo kidogo kilichopo karibu na
hapo walikuta kituo hicho kimefungwa na kufuri na hakuna askali yoyote
lakina baada ya muda askali polisi mmoja alitokea.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment