Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Bi. Pamela Said akiwa katika maumivu makubwa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ilibainika kuwa siku hiyo majira ya saa 5:00 usiku, Alex, akiwa amepitiwa na usingizi simu yake iliita huku jina la Salima likionekana kwenye ‘skriini’.
 
Ilisemekana kwamba Salima aliwahi kuwa mfanyakazi katika pub yao ambapo Pamela alimtuhumu kuwa na uhusiano na mumewe.
Bw. Alex, mume wa Pamela Said.
Ilidaiwa kuwa Pamela alimuomba mumewe wakamtimua kazi Salima lakini amekuwa akiendeleza uhusiano huku akipiga simu mara kwa mara hasa usiku kitendo ambacho kilimchukiza Pamela. 
 
Ilidaiwa kuwa baada ya kuona simu hiyo, Pamela alimuamsha mumewe ambaye alipokea simu hiyo na kuanza kujikanyaga na kukata simu ndipo alipompigia kwa namba yake na kuanza kujibizana huku akipokea maneno ya karaha bila kutegemea mazungumzo hayo yalimtia hasira Pamela ambaye alimuuliza kwa hasira mumewe huku akitaka kujua kuna nini kati yake na huyo Salima.
Pamela Said na mumewe Alex wakati wa harusi yao.
Ilielezwa kuwa kitendo hicho cha mke kutaka kujua ukweli ndipo mumewe akaanza kutoa maneno akidai kwamba atamuonesha kazi ambapo alichukua mchi wa kinu na kuanza kumpiga nao maeneo ya usoni na mikononi hadi Pamela akapoteza fahamu.
 
Ilisemekana kuwa kelele za kipigo hicho kiliwashtua majirani ambao walisogea kwenye nyumba hiyo ili kujua nini kinaendelea na kumkuta Pamela akiwa amezimia jambo lililowafanya kutafuta msaada wa kumpeleka hospitali ili kuokoa maisha yake.
Pamela Said na Bw. Alex wakati wakifunga ndoa.
Ilidaiwa kwamba katika hali isiyo ya kawaida, mume wa Pamela alikataa na kuwaambia wampeleke hospitali wenyewe, kwa kuwa kulikuwa na gari ikabidi wamtafute dereva usiku huo na kumwahisha kwenye ‘dispensari’ ya karibu iitwayo Kwa-Jose.
 
Baada ya kumfikisha dispensari walikataliwa kutokana na hali ya Pamela kuwa mbaya hivyo wakamkimbiza kwenye zahanati inayoitwa Jeshi, napo walishauri mgonjwa huyo apelekwe Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Pamela alifikishwa Muhimbili alfajiri ya saa 12:00 akiwa anatapika damu katika hodi ya Mwaisela na kuanza matibabu kisha kutoa taarifa katika Kituo cha Sitaki-Shari na kufunguliwa jalada la kesi namba STK/RB/70220/2014- SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
Habari kutoka kwa mmoja wa ndugu wa Pamela zilieleza kuwa kulitokea mvutano mkubwa wa pande mbili ambapo Alex alitaka mke arudishwe nyumbani na kuendelea na matibabu jambo ambalo lilipingwa vikali na kaka wa Pamela akisema dada yake bado ana hali mbaya.

Akizungumza kwa tabu hospitalini hapo, Pamela alikiri kufanyiwa ukatili huo na mumewe.
Credit GPL 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top