Wanawake wanne raia wa Rwanda wametiwa
mbaroni mjini Dodoma kutokana na kuingia
nchini kinyemela na kujihusisha na biashara
ya ukahaba.
Watuhumiwa watatu kati ya hao, Saidat
Umotoni (28), Asha Abimana (25) na Asia
Umotoni Wase (30), hii ni mara yao ya pili
kukamatwa mjini hapa wakidaiwa kujihusisha
na biashara hiyo.
Mara ya kwanza ilikuwa Novemba mwaka jana
ambapo wote ( Asia, Asha na Saidat) baada ya
kukamatwa, walirudishwa kwao baada ya
kulipa faini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana
Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma,
Proches Kuoko, alimtaja mwingine
aliyekamatwa ni Chalote Uwase (28) ambaye
ameshahukumiwa kifungo cha miaka miwili
anachotumikia katika Gereza la Isanga, mjini
hapa.
Alisema wahamiaji hao wote kwa pamoja
walikamatwa na maofisa wa kikosi cha
Uhamiaji, baada ya kupata taarifa kwa kuwepo
raia hao katika eneo la barabara ya Bahi ndani
ya Manispaa ya Dodoma.
Alisema wanawake hao walikamatwa usiku
kwenye mitaa hiyo huku wakiwa kwenye
harakati za kutafuta wateja na walipohojiwa
wote kwa pamoja hawakuwa na hati ya
kusafiria na kuishi hapa nchini na
walizokuwanazo zilikuwa zimeisha muda wake
wa matumizi.
“Hata walipopekuliwa, walikutwa wakiwa na
hati ya kusafiria iliyokuwa imeisha muda wake
wa kuwawezesha kuishi hapa nchini na
walipohojiwa zaidi walisema wao kazi yao ni
uchangudoa,” alisema Kuoko.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment