Amina anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba OB/RB/9967/2014.
Akisimulia masahibu yaliyompata akiwa katika Wodi Namba Tatu ya hospitali hiyo, Yusta alisema: “Nililetwa Dar es Salaam mwaka 2010 kufanya kazi za nyumbani baada ya bosi wangu (Amina) ambaye ni binamu yangu kuzungumza na mama yangu na kuniomba nije kumsaidia kazi ndogondogo.”Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.
Binti
huyo, mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika Kijiji cha Kampala amedai kuwa
amekuwa akiteswa na kufungiwa ndani ya nyumba na tajiri yake, Amina
Maige wa Mwananyamala, Kwa Manjunju katika kipindi chote hicho.Alisema
aliishi vizuri na mwajiri wake huyo, lakini mwaka 2012 ndipo mambo
yalipoanza kubadilika akidai kuwa Amina alianza kumwadhibu kwa kumng’ata
na kumchoma kwa pasi kila alipomtuhumu kutokufanya kazi zake vizuri.
“Alikuwa
akinichapa na kuning’ata sehemu mbalimbali wakati mwingine usoni, pia
kunichoma kwa pasi yenye moto kila aliponituhumu kutokufagia au kupiga
deki vizuri.”
Hakuwahi kupelekwa hospitali
Alisema
licha ya kupata vidonda kutokana na adhabu hizo, mwajiri wake huyo
hakuwahi kumpeleka hospitali na pale alipoona hali ni mbaya alimnunulia
dawa… “Tunaishi wawili tu baada ya kuondoka mumewe na mtoto wake
kumpeleka shule ya bweni… niliugulia hadi nikapona bila mtu mwingine
kufahamu.”
“Akienda
kazini anafunga geti na kunikataza kufungua hata kama mtu atagonga…
sokoni nilikuwa naenda siku ambazo yeye yupo tu na huwa akiniamrisha
niende haraka na kurudi pasipo kuzungumza na mtu yeyote.”
Alisema
mwajiri wake huyo alikuwa akituma pesa za mshahara wake kwa mama yake
akisema ndiye anayepaswa kulipwa, jambo ambalo anadhani limemfanya mama
yake kuhisi mwanaye yuko katika mikono salama… “Kila alipotuma alipiga
simu na kunipa niongee na mama kuhakikisha kama zimefika huku
akinisimamia na baada ya hapo anachukua simu.”
Ataka kurudi kwao
Binti
huyo ambaye sehemu kubwa ya mwili wake ina alama za kung’atwa meno na
majeraha ya kuchomwa na pasi, alisema: “Ninaomba mtu yeyote mwenye hela,
nataka nikitoka hapa hospitali nirudi Tabora kwa mama. Nina shaka na
maisha yangu hapa kwa huyu mama… sitaki tena kubaki Dar es Salaam
kutokana na mateso ninayoyapata.”
Polisi wasema
Mkaguzi
Msaidizi wa Dawati la Jinsia Polisi Mkoa wa Kinondoni, Prisca Komba
alisema taarifa za binti huyo ziliwafikia baada ya majirani kupeleka
taarifa hizo katika Kikundi cha Kipange kilichopo Kwa Manjunju ambacho
nacho kilitoa taarifa polisi na ndipo mtego wa kumnasa mwanamke huyo
ukawekwa.
Majirani
walichukua hatua hiyo kutokana na kusikia kelele za kilio mara kwa mara
zikitokea ndani ya nyumba ya mtuhumiwa. “Tumekagua makovu na majeraha
mbalimbali yaliyo katika mwili wake na kupata jumla kuwa yako 91,”
alisema Komba na kuongeza:
“Toka
jana amekuwa akinitaka nisiondoke mbali naye amekuwa na hofu, lakini
sasa afadhali kidogo baada ya kumpatia ushauri na kumhakikishia kwamba
hapa yuko salama.”
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Thobias Edoyeka alisema suala hilo
linashughulikiwa na polisi pamoja na ustawi wa jamii, kauli iliyoungwa
mkono na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mwananyamala, Rose Temu ambaye alisema
wanafuatilia kwa karibu matibabu yake pamoja na usalama wake. “Hali
yake ikishaimarika na kujiridhisha kuwa anaendelea vizuri, tutakuwa na
jukumu la kumuunganisha na familia yake,” alisema.
Ofisa Muuguzi Msaidizi Wodi Namba Tatu ambayo ni ya kinamama, Rose Mussa alisema Yusta anaendelea vizuri.
“Anaendelea
vizuri kwa kweli, jana (juzi) hakuwa hivi alikuwa mwoga hawezi
kujieleza tofauti na leo (jana)… bado anaendelea na vipimo, tutakapoona
anafaa kuruhusiwa tutafanya hivyo na kumkabidhi kwa ustawi wa jamii.”
Credit: Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment