Majonzi na simanzi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson’ katika Viwanja vya Leaders.
WAKATI jana jiji la Dar likizizima kwa vilio, majonzi na simanzi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwongoza filamu za Kibongo, marehemu George Otieno Okumu ‘Tyson’ nchini kwao Kenya ni zaidi ya msiba.
Tyson
aliagwa na mastaa, mashabiki na wadau wa burudani Bongo kwenye Viwanja
vya Leaders Kinondoni, Dar kabla ya mwili wake kusafirishwa kwa ndege
kwenda Kenya kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Kisumu nchini humo
keshokutwa Jumamosi.
Mbali na Wabongo, pia kulikuwa na
Wakenya ambao walitumia nafasi hiyo kumuaga mwenzao ambapo baadhi yao
waliambatana na mwili huo kwenda Kenya.
Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu
ulipelekwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),
Dar tayari kwa safari ya Kenya.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mwili wa
marehemu ulipokewa kwa majonzi makubwa na ndugu, jamaa, marafiki, mastaa
na watu mbalimbali kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi
nchini humo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya
nchini humo hasa redio, mitandao ya kijamii na ‘blogi’ vilieleza kwa
simanzi kubwa juu ya kifo cha Tyson kwani kabla ya kujikita Tanzania
mwaka 2000 alikuwa akifahamika kama bondia matata ndiyo chanzo cha
kupewa jina la Tyson nchini humo.
Baadhi ya vyombo vilivyoripoti na
kusababisha Kenya kuzizima kwa vilio ni pamoja na Radio Citizen, Citizen
Television, mitandao ya Kenya.co.ke, mseto.co.ke, Ghafla.co.ke na
mingine kibao.
“Kusema kweli kwa hapa Nairobi, Tyson
alikuwa akifahamika sana. Unajua watu wengi walikuwa hawaamini lakini
baada ya mwili kuwasili ndiyo wameamini.
“Hata ndugu walikuwa hawaamini hadi
walipoona jeneza na kuhakikishiwa kuwa limebeba mwili wa mpendwa wao,”
alisema shuhuda wetu kutoka Jiji la Nairobi.
Baada ya kufikishwa Nairobi, ndipo
taratibu za kuupeleka mwili huo zikaanza ambapo utapumzishwa kwenye
nyumba ya milele Kisumu Jumamosi ijayo.
Tyson alifanya kazi nyingi Bongo ikiwa
ni pamoja na kufungua milango ya Bongo Movies alipotengeneza kwa mara
ya kwanza Filamu ya Girlfriend na baadaye ikifuatiwa na Dilemma.
Pia alikuwa mwongozaji wa vipindi
mbalimbali runingani kuanzia ITV, EATV na TV1. Alipatwa na mauti maeneo
ya Gairo, Morogoro baada ya kutokea ajali mbaya akitokea Dodoma
kutengeneza Kipindi cha Mboni Show cha EATV chini ya mwanadada Mboni
Masimba.
Wakati wimbi la vifo vya wasanii
likiongezeka, katika hali ya kushtua, mtabiri na mnajimu maarufu Bongo,
Maalim Hassan Yahya Hussein ameendelea kusisitiza kuwa utabiri juu ya
vifo vya mastaa utaendelea hadi mwezi Aprili, mwakani.
Akizungumza na waandishi wa Global
Publishers kwenye makao makuu ya gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar,
Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mnajibu Afrika na kwingineko
duniani, marehemu Shehe Yahya Hussein alisema:
“Nasisitiza tena, mwezi wa kinyota
huanza Aprili na kuishia Aprili. Katika kipindi cha mwaka huu, kinyota
inaonesha watakufa wasanii mfululizo hivyo ni vema wakachukua tahadhari
na kukubaliana na hali halisi.”
Alipoulizwa nini cha kufanya, Maalim Hassan aliendelea:
“Wasanii wanatakiwa kumuomba Mungu.
Kama ni Muislam asikose kuswali msikitini, kama Mkristo asikose
kuhudhuria kanisani na kama ni mpagani, basi atafute namna yake ya
kumuomba mungu wake.”
Mbali na Mungu, Maalim alikwenda
mbele zaidi: “Pia kinyota wasanii wasivae nguo nyekundu kabisa. Wasipake
rangi nyekundu midomoni (lipstick) na kwenye kucha zote. Kimsingi
waachane na vitu vya rangi nyekundu.
“Pia wasitoke kwenda kwenye starehe
au shughuli za usiku hasa Jumanne na Jumamosi jioni kwani ni siku za
vita kati sayari ya Venus na Mercury ambapo mkuu wake ni Israeli Mtoa
Roho.”
Alisema kuwa suala la vifo vya
wasanii si kwa Tanzania tu kwani hivi karibuni tasnia ya filamu duniani
imekuwa ikiondokewa na wasanii kibao kuanzia Hollywood (Marekani),
Nollywood
(Nigeria), Bollywood (India) na hata nchini Kenya mwigizaji aliyeigiza
kama Idd Amin kwenye simema ya Rise and Fall of Idd Amin amefariki dunia
hivi karibuni hivyo ndiyo hali halisi kwa kipindi hiki hadi Aprili,
mwakani.
Mbali na Tyson anga la bururudani
Bongo liliwapoteza wasanii wengine kama Shaila Haule ‘Recho’ Adam
Philip Kuambiana na Amina Ngaluma.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
Picha na GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment