Seke
seke la usajili wa kiungo wa kimataifa wa Spain anayekipiga katika
klabu ya FC Barcelona ya La Liga limechukua hatua nyingine jana usiku.
Fabregas
ambaye anapiganiwa na vilabu vya Arsenal, Manchester United na Chelsea
anatarajiwa kuuzwa baada ya kocha wake mpya Luis Enrique kuripotiwa
kutokuwa na mpango nae kwenye utawala wake mpya Camp Nou.
Huku vita
kubwa ikiwa inaendelea miongoni mwa vilabu vinavyomtaka, jana kwenye
mkutano wa waandishi wa habari wa timu ya taifa ya Spain inayojiandaa na
michuano ya kombe la dunia, beki na mchezaji mwenzie Fabregas, Gerard
Pique alisikika akimwambia kocha mkuu wa timu ya taifa ya Spain kwamba
Cesc anaondoka Barcelona, na taarifa hizo ameambiwa na Fabregas
mwenyewe.
Mazungumzo
ya Pique na Del Bosque yalifanyika dakika chache kabla ya kuanza kwa
mkutano, huku wakiwa hawajui kwamba vipokea sauti vimeawashwa wakawa
wanazungumzia uhamisho wa Cesc.
Pique alisikika akisema: “[Cesc Fabregas] ameniambia uhamisho umekamilika, ameniambia amenunuliwa kwa €33million.”
Del Bosque akamjibu: “Maskini yule Rais Poor (akimaanisha Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu). Hawezi kushinda namna.”
Katika mazungumzo hayo wawili hao hawakuitaja timu ambayo Fabregas ataenda kati ya timu zinazomtaka.
Angalia mazungumzo hayo hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment