Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Wazee wawili akiwemo mlinzi mmoja wa ofisi ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Bunda,
mkoani Mara, wamefikishwa mahakamani kwa
kosa la kulawiti wanafunzi sita wa shule za msingi
zilizoko wilayani hapa.
Waliofikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya
Bunda, ni pamoja na Thomas Machugu (72)
ambaye ni mlinzi na mkazi wa mtaa wa Saranga.
Mwingine ni Salum Mfumbasi (66) ambaye ni
mfanyakazi wa ndani kwa mfanyabiashara mmoja
wa mjini Bunda.
Watuhumiwa hao walifikishwa juzi katika
mahakama hiyo mbele ya hakimu, James Manota
na kusomewa mashitaka yao na mwendesha
mashitaka wa polisi Masood Mohammed.
Akiwasomea mashitaka yao, Mohammed alisema
washitakiwa hao wote kwa pamoja waliwalawiti
wanafunzi hao, ambao umri wao ni kati ya miaka
10 na 13 kwa tarehe na muda tofauti, katika
maeneo mbalimbali mjini hapa.
Alisema kuwa polisi waliwagundua watu hao
baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na
kwamba baada ya kuwahoji watoto hao walisema
kila kitu jinsi washitakiwa hao wamekuwa
wakiwaingilia kwa zamu, pindi wanapokwenda
shuleni baada ya kupita katika maeneo hayo.
Aidha, aliongeza kuwa baada ya watoto hao
kupelekwa hospitalini na kufanyiwa uchunguzi wa
kitabibu ilibainika kuwa walikuwa
wamekwishaharibiwa sehemu zao za siri.
Washitakiwa wote kwa pamoja wamekana
mashitaka yao na kupelekwa mahabusu hadi Mei
22 mwaka huu, kesi yao itakapotajwa tena
mahakamani hapo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top