Simanzi kubwa imetanda katika Kijiji cha Roo,
Kata ya Masama Mashariki wilayani Hai,
Kilimanjaro, baada ya kijana mwenye umri wa
miaka 32 kuwaua wazazi wake wawili kwa
kutumia panga na shoka, kisha kuchoma moto
nyumba yao.
Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Yusuph
Njau aliwaua wazazi wake, Shahidu Njau (60) na
Minae Swai (57) baada ya kuwafungia ndani na
kuwakata kata kwa kutumia shoka na panga.
Akizungumza na mwandishi, Diwani wa Kata ya
Masama Mashariki, Ally Mwanga alisema mauaji
hayo yalitokea juzi majira ya saa 12: 30 jioni,
katika nyumba waliyokuwa wanaishi wanafamilia
hao.
Mwanga alisema baada ya kijana huyo kufanya
mauaji hayo, alichukua uamuzi wa kuchoma
nyumba huku miili ya wazazi wake ikiwa ndani,
ambapo majirani walitoa msaada wa kudhibiti
moto huo baada ya kuona moshi ukifuka ndani.
Alisema wakati wananchi wakiendelea kuudhibiti
moto huo, ndipo waliona miili ya marehemu ikiwa
inavuja damu, hali iliyosababisha kutoa taarifa
Polisi.
Alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya matukio
hayo na kwamba maziko ya wazazi wake
yalitarajiwa kufanyika jana jioni kijijini kwao Roo.
Mwanga alisema taarifa za awali zilizopatikana
kuhusiana na tukio hilo kuwa chanzo ni matumizi
ya dawa za kulevya na bangi ambazo amekuwa
akitumia kwa muda mrefu kijana huyo.
“Hili tukio ni la kutisha sana, linahuzunisha sana,
kijana huyu amekuwa akitumia dawa za kulevya
kwa muda mrefu, hivyo kichwa kimeathiriwa kwa
matumizi hayo,” alisema Mwanga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Roo,
Khalfan Swai, alilieleza kuwa kijana huyo amekuwa
na matukio ya kutishia watu hapo kijijini, na
amewahi kufungwa kwa muda baada ya kuwapiga
baba mdogo na shangazi yake.
Swai alisema kijana huyo amekuwa akitembea na
shoka na panga kwa kuwatishia watu, lakini
wazazi wake walikuwa wakimtetea kuwa mwana
wao hahusiki na vurugu zozote za kutishia watu.
Pia alisema kijana huyo awali alikuwa anaishi Dar
es Salaam akiwa anajifunza ngumi za kulipwa,
lakini baada ya kuathirika na matumizi ya dawa
za kulevya ndipo aliporejea kijijini.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert
Boaz akitoa
taarifa za tukio hilo, alisema Jeshi la Polisi
linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa,
ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
VIA MZALENDO
KIJANA AUA WAZAZI WAKE WAWILI KISHA KUICHOMA MOTO NYUMBA YAO HUKO KILIMANJARO
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment