Watalii wengi hutembea nusu uchi wakati wanapotembelea fuzo za bahari
Serikali ya Qatar imezindua
kampeini ya kuwasihi watalii kuvalia mavazi ya heshima wanapokuwa katika
maeneo ya umma na pia kuheshimu maadili ya kiisilamu nchini humo.
Kupitia kwa Twitter na Instagram, serikali hiyo
inaweka picha zinzoonyesha ambavyo watalii wanapaswa kuvalia wakiwa
nchini humo pamoja na kuonyesha mavazi yasiyoruhisiwa.
Qatar:Onyo kwa watalii wanaovalia vinguo vifupi

Mavazi kama nguo fupi, zisizo na mikono mirefu na vitopu vifupi, yameharamishwa, wakati wanaume hawaruhusiwi kuvalia kaptula na vesti huku wakionyesha vifua vyao.
Kauli mbiu ya kempeini hiyo ni'' Ukiwa Qatar wewe ni mmoja wetu. Tusaidie kuendeleza maadili na utamaduni wa Qatar , tafadhali valia mavazi ya heshima. ''
Kampeini hiyo inawaomba watu kufunika mabega yao na magoti na kujizuia kuvalia stockings.
Kituo cha utamaduni wa Qatar, kimewahi kuzindua kampeini kama hii ili kuwafunza watalii kuhusu mavazi yao.
"hatutaki watoto wetu kuishi katika mazingira kama haya na kuweza kujifunza mambo yasiyokubalika na ndio maana tunafanya kampeini hii. ''
Qatar, ni mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 na ina takriban watu milioni 2 na pia hutumia sheria ya kiisilamu katika mfumo wake wa sheria.
Raia wa Uingereza 17,500, wanaishi katika nchi hiyo na nchi hiyo pia hupokea wageni 40,000 kila mwaka.
Kuvalia nguo zinazoonekana kukosa heshima ni kinyume na sheria sawa na ilivyo kutoa matamshi ya matusi au kufanya kitendo chochote kisichokubalika katika sehemu ya umma.
Ikiwa atapatikana na hatia mtu anaweza kufungwa jela miezi sita au kutozwa faini.
Chanzo bbc
BOFYA HAPA LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

Mavazi kama nguo fupi, zisizo na mikono mirefu na vitopu vifupi, yameharamishwa, wakati wanaume hawaruhusiwi kuvalia kaptula na vesti huku wakionyesha vifua vyao.
Kauli mbiu ya kempeini hiyo ni'' Ukiwa Qatar wewe ni mmoja wetu. Tusaidie kuendeleza maadili na utamaduni wa Qatar , tafadhali valia mavazi ya heshima. ''
Kampeini hiyo inawaomba watu kufunika mabega yao na magoti na kujizuia kuvalia stockings.
Kituo cha utamaduni wa Qatar, kimewahi kuzindua kampeini kama hii ili kuwafunza watalii kuhusu mavazi yao.

Picha zinazotumiwa na Qatar kuhamasisha watalii dhidi ya kuvalia nguo zisizo na heshima
"kiwango cha watu kuvalia nguo zisizo za
heshima, kimeongezeka hasa katika maeneo ya umma ikiwemo katika maduka
makubwa ya kifahari,'' alisema Nasser Al Maliki, afisaa mkuu wa
mawasiliano katika kituo hicho."hatutaki watoto wetu kuishi katika mazingira kama haya na kuweza kujifunza mambo yasiyokubalika na ndio maana tunafanya kampeini hii. ''
Qatar, ni mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 na ina takriban watu milioni 2 na pia hutumia sheria ya kiisilamu katika mfumo wake wa sheria.

Raia wa Uingereza 17,500, wanaishi katika nchi hiyo na nchi hiyo pia hupokea wageni 40,000 kila mwaka.
Kuvalia nguo zinazoonekana kukosa heshima ni kinyume na sheria sawa na ilivyo kutoa matamshi ya matusi au kufanya kitendo chochote kisichokubalika katika sehemu ya umma.
Ikiwa atapatikana na hatia mtu anaweza kufungwa jela miezi sita au kutozwa faini.
Chanzo bbc
BOFYA HAPA LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment