
MTOTO
Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne mkoani
Morogoro, sasa anaopumulia mashine katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili
Nasra,
alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipohamishiwa Mei 26
mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea katika Hospitali ya mkoa
wa Morogoro.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa
Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu alisema Nasra, aliwekewa
mashine maalum ili kusaidia kupata hewa ya Oksijeni baada ya kuanza
kupumua kwa shida.
Alibainisha
kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea vizuri lakini juzi usiku
ilibadilika na hivyo kuwekewa mashine ya kupumulia.
Dk. Kombo
alisema kutokana na hali hiyo, madaktari wa zamu juzi waliamua
kumfanyia vipimo na kubaini anasumbuliwa na Ugonjwa wa Nemonia.
Dk.
Kombo, alisema mtoto huyo akipata nafuu ya ugonjwa wa Nemonia,
ataendelea na vipimo vikubwa vya mwili mzima ikiwamo moyo na figo.
Alisema
licha ya ya kumpatia dawa za Nemonia, wanaendelea kumpatia chakula na
dawa baada ya vipimo vya awali kubaini ana Utapiamlo.
Ofisa
Muuguzi wa zamu, Iluminata Sokani, alisema licha ya kupumulia mashine
hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika kila wanapomfanyia vipimo kujua
maendeleo yake.
Naye mama
mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla ya mtoto hajawekewa
mashine ya kumsaidia kupumua, alimuambia anaumia kifuani na kiunoni
Mtoto
Nasra alifichuliwa na Mei 2, mwaka huu na majirani ambao walimweleza
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Dia Zongo kuwa alikuwa
amefichwa katika boksi na Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu
Said mkazi wa Kata hiyo mkoani Morogoro.
Majirani
hao walimweleza Zongo kuwa Nasra alifichwa ndani ya boksi tangu akiwa na
umri wa miezi tisa 2009 na kwamba hafanyiwi usafi wala kumtoa nje.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment