Zeidan alitoa wito kwa Marekani kusaidia Libya kupambana na wapiganaji wa kiisilamu
Waziri mkuu wa Libya ametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami kutoka nyumbani kwake mjini Tripoli.
Duru zinasema kuwa bwana Ali Zeidan ametekwa
nyara na kupelekwa katika eneo lisilojukana , lakini hakuna taarifa
zaidi kuhusu tukio hilo.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda Zeidan amezuiliwa.
Kundi lililokuwa la waasi na ambalo lina
uhusiano na serikali limekiri kumteka nyara Zaidan kufuatia kibali cha
kumkamata kilichotolewa na kiongozi wa mashtaka .
Picha ya Zeidan akitekwa nyara mjini Tripoli
Lakini serikali ya Libya imekanusha madai hayo.
Kituo cha televisheni cha Al Arabiya kimeonyesha picha za bwana Zaidan
akitekwa nyara.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema Zeidan alitekwa nyara akiwa ndani ya hoteli ya kifahari anamoishi.
Serikali imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kali
baada ya makomando wa Marekani kumkamata mmoja wa viongozi wa al-Qaeda
Anas al-Liby nchini Libya.
Bwana Liby alikamatwa Jumamosi mjini Tripoli kwa
madai ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya
balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 2008.
Mnamo siku ya Jumatatu Libya ilimhoji balozi wa Marekani kuhusu kukamatwa Al Liby.
Kwa upande wake Zeidan alitoa wito kwa Marekani
na nchi za Magharibi kuisaidia serikali ya Libya kukomesha vitendo vya
wapiganaji wenye itikadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi yake inatumia
kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya
kanda hiyo.
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/06/130506102008_libya_pm_304x171_ap.jpg)
Zeidan alitoa wito kwa Marekani kusaidia Libya kupambana na wapiganaji wa kiisilamu
Waziri mkuu wa Libya ametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami kutoka nyumbani kwake mjini Tripoli.
Duru zinasema kuwa bwana Ali Zeidan ametekwa
nyara na kupelekwa katika eneo lisilojukana , lakini hakuna taarifa
zaidi kuhusu tukio hilo.Kundi lililokuwa la waasi na ambalo lina uhusiano na serikali limekiri kumteka nyara Zaidan kufuatia kibali cha kumkamata kilichotolewa na kiongozi wa mashtaka .
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/10/131010074901_zaidan_taken_304x171_bbc_nocredit.jpg)
Picha ya Zeidan akitekwa nyara mjini Tripoli
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema Zeidan alitekwa nyara akiwa ndani ya hoteli ya kifahari anamoishi.
Serikali imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kali baada ya makomando wa Marekani kumkamata mmoja wa viongozi wa al-Qaeda Anas al-Liby nchini Libya.
Bwana Liby alikamatwa Jumamosi mjini Tripoli kwa madai ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 2008.
Mnamo siku ya Jumatatu Libya ilimhoji balozi wa Marekani kuhusu kukamatwa Al Liby.
Kwa upande wake Zeidan alitoa wito kwa Marekani na nchi za Magharibi kuisaidia serikali ya Libya kukomesha vitendo vya wapiganaji wenye itikadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi yake inatumia kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya kanda hiyo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment