Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager akiwa na baadhi ya wasanii
watakaoshiriki katika Kilimanjaro Music Tour iliyozinduliwa Jijini Dar
es Salaam. Ziara hii inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager,
itafanyika kuanzia mwezi huu hadi Agosti mwaka huu katika mikoa 10.
KILI MUSIC TOUR KULETA MSISIMUKO MIKOANI
MEI 13, 2014: Bia
ya Kilimanjaro Premium Lager imeandaa ziara maalumu ya wasanii maarufu
kama Kili Music Tour 2014 ni ziara maalum ya wasanii maarufu zaidi ya 30
ambao watatoa burudani kwenye mikoa isiyopungua 10 hapa nchini kuanzia
mwezi Mei hadi Septemba 2014 lengo ikiwa ni kupeleka muziki wa Tanzania
kwenye kilele cha mafanikio.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bw. George Kavishe alisema Kili
Music Tour 2014 itahusisha mikoa ya Moshi, Mwanza, Kigoma, Kahama,
Iringa, Mbeya, Dodoma, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam.
“Ziara
hii itaanzia Mkoani Moshi Mei 24, Mwanza Mei 31, Kahama Juni 7, Kigoma
Juni 14, Iringa Juni 21, Mbeya Agosti 9, Dodoma Agosti 16, Tanga Agosti
23, Mtwara Agosti 30, Dar es Salaam Septemba 6,” alisema Kavishe.
Wasanii
watakaotoa burudani ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz, Linex, Professor
J, Izzo Biznez, Kala Jeremiah, Fid Q, Snura, Weusi, Ben Paul, Mzee
Yusuph, Shilole, Mwasiti, Ney wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Juma
Nature, Warriors, Madee, Young Killer, Jambo Squad, AY, Venessa Mdee,
Mashujaa Band, Rich Mavoko, Chriatian Bella.
Bw.
Kavishe alisema lengo la Kili Music Tour 2014 ni kupeleka wasanii
kwenye sehemu ambazo aina za muziki wao na mitindo yao inakubalika zaidi
ili kuwapa wananchi fursa ya kuwaona wasanii hao moja kwa moja.
“Hii
pia ni fursa kwa wasanii kuweza kutambulisha kazi zao katika mikoa hiyo
na hatimaye kuongeza fursa kwa mauzo na kukubalika katika mikoa hiyo,”
alisema.
Kwenye
kila mkoa ambapo litafanyika tamasha, wasanii wanaochipukia kutoka
mikoa hiyo watapewa fursa ya kutumbuiza katika utangulizi. Hii ni
kuwajengea uwezo wa kujiamini na pia hili litakuwa ni jukwaa la
kuonyesha vipaji vyao.
Kili
Music Tour itatangazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kupitia
promosheni ambazo zitafanyika katika mikoa yote husika.
“Kili
Music Tour itakuwa ni burudani kubwa ya aina yake kutokana na motisha
zilizoandaliwa ili kuhakikisha wasanii wako katika hali na mazingira
mazuri kuweza kutoa burudani yenye kiwango bora,” alisema Bw Kavishe.
Ziara hii itaratibiwa na East Africa TV na Radio, Executive Solutions na Integrated Communications.
ENDS
Michael MukunzaMedia Manager Executive Solutions Limited Plot 74 Block 45B, Executive Junction Ali Hassan Mwinyi Road P O Box 1601, Dar es Salaam Mob 1: +255 776978302 l Mob 2: +255 714683451 l Fax: +255 22 2122027 Email: m.mukunza@ |
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment