

Kaburi la Sheikh Yahya Hussein ambaye alizikwa tarehe
21.5.2011.Makaburi
mawili ya Sheikh Yahya Hussein na Sheikh Kaseem Bin Jumaa yamevunjwa na
mgambo wa jiji saa nane usiku eneo la Tambaza, makaburi ambayo yana
muda mrefu katika eno hilo.
Hata hivyo haijajulikana chanzo cha kuvunjwa kwa makaburi hayo.
Wakiongea na waandishi wa habari baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya
vyakula eneo hilo wamedai kuwa, walifika asubuhi na kukuta hali hiyo ya
kuvunjwa kwa vibaraza vya maduka yao pamoja na kuvunjwa kwa makaburi
hayo mawili ya watu masheikh mashuhuri hapa nchini.
Naye
mtoto wa marehemu Sheikh Yahya Hussein, Bi. Mariam Hussein alifika
katika makaburi hayo na kujionea kwa macho yake jinsi kaburi la Baba
yake lilivyobomolewa.
Mariam amesema anasikitishwa sana kwa kuvunjwa kwa kaburi la Baba yake bila ya sababu ya msingi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro










Post a Comment
Post a Comment