Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Ukisikia paaa! Mastaa vidume wa Bongo Movies, William Mtitu na Zuberi
Mohamed ‘Niva’ wanadaiwa kutoelewana na kuzichapa kavukavu kabla ya
kuamuliwa na watu waliokuwa nao kwenye mandhari ya kurekodia sinema
(location).
Kwa mujibu wa sosi wa tukio hilo lililojiri maeneo ya Kijichi jijini
Dar, hivi karibuni, kisa cha wawili hao kutupiana maneno makali kisha
kukamatana ni msichana aliyetajwa kwa jina moja la Happy ambaye ni
‘sekretari’ wa Mtitu anayedaiwa kutoka kimalavu na Niva.
Sosi huyo alieleza kwamba Mtitu na wasanii wengine walikuwa
wakirekodi filamu ya mwigizaji mwenzake, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ambapo
Niva alikwenda kuwatembelea hivyo akaombwa gari lake litumike kwa muda
wakati yupo hapo.
Ilisemekana kuwa Niva alilala hukohuko, kitendo kilichomshtua mpenzi
wake Happy, kwani baada ya kutomuona nyumbani, kesho yake aliamua
kumfuata mwanaume wake aliyekuwa ‘location’.
“Sababu ya ugomvi ni Mtitu, naye alienda huko location na bahati
akamkuta Niva, akamuuliza kama mpenzi wake huyo alilala huko, kitendo
ambacho ilionekana wazi kuwa Mtitu hakupenda kwani alimtishia Niva kuwa
atahakikisha amemfukuza kazi mpenzi wake huyo,” alisema sosi huyo.
Sosi huyo alidai kwamba ugomvi ulikuwa mkubwa hadi Mtitu akainua simu
na kumwambia Happy asikanyage tena ofisini kwake huku akimtaka Niva
kutofika ofisini kwake kwani atavunja gari lake.
Baada ya ushu hiyo kujaa tele kwenye dawati letu, wanahabari wetu walimwendea hewani Niva ambaye alikiri kutokea kwa tatizo hilo na kudai kuwa Mtitu ni mkorofi kwani amekuwa akigombana na kila mtu.
“Mimi ninashangazwa sana na Mtitu kwani ishu binafsi anaziingiza
kwenye kazi, sasa amemfukuza kazi mpenzi wangu Happy kisa tu mimi na
yeye tulipishana kauli lakini inawezekana kuna kitu nyuma ya pazia
ambacho ninakifanyia uchunguzi bado,” alisema Niva.
Kwa
upande wake, Mtitu alisema ni kweli alitofautiana na Niva kwani hana
heshima kutokana na kumjibu na kumtukana kwa sababu ya mwanamke wake
ambaye ni sekretari wake na kuamua kumsimamisha kazi.
“Niva hana heshima halafu ni mtoto mdogo sana kwangu, alinikosea,
kuna vitu vibaya alivifanya yeye na huyo mwanamke wake ndiyo maana
nimeamua kumsimamisha kazi hadi nikimaliza kushuti ndipo nitakaa na huyo
sekretari wangu na kumweleza kinagaubaga kuhusu kuwa na nidhamu
kazini,” alisema Mtitu.
>>>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro









Post a Comment
Post a Comment