- Ampongeza kwa ujenzi wa madaraja matatu makubwa, Daraja la Malagarasi,Kilombero na Daraja la Kigamboni.
- Ujenzi wa Sekondari za Kata
- Nape awaambia wakazi wa kijiji cha Mahembe wachague viongozi watakaotatua matatizo yao ya msingi kwanza na si vinginevyo kwani takwimu zinaonyesha viongozi wengi wa upinzani wameshindwa kutatua matatizo ya wananchi wa majimbo wanayoyaongoza.
- Wanachama wapya 160 na 7 kutoka upinzani wajiunga na CCM
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kigoma
Vijijini na kuwataka kufanya kazi kwa umoja na mshikamano .
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Kigoma Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kigoma Vijijini akiwa pamoja
na kiongozi wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Wilaya hiyo Ndugu
Mgaya Mustafa ambaye alitoa taarifa ya kuwepo kwa kero ya kukamatwa
Daladala kwa sababu ya kukosa sare za dereva na kondakta ambazo kwa
maelezo ya madereva hao tatizo lipo kwa aliyepewa tenda kuchelewesha
kushona.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkungwe kata ya Mahembe
wilaya ya Kigoma Vijijini na kuwaambia Chama Cha Mapinduzi kiahidi
kinachoweza kutekelezeka hivyo ahadi ya kuwapatia maji wanakijiji hao
ipo na mkandarasi alishajenga mradi kwa asilimia 70 hivyo watapata maji
mapema iwezekanavyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akiangalia mradi wa maji katika kijiji cha Mkungwe kata ya
Mahembe wilaya ya Kigoma Vijijini
Kijiji cha Mkungwe wilaya ya Kigoma Vijijini kupata maji safi na salama hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akihutubia wakazi wa kijiji cha Mahembe ambapo alitoa sifa kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kujenga
madaraja makubwa matatu,Maragarasi ,Kilombero na Kivukoni na kujenga
Shule za Kata nchi nzima.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro















Post a Comment
Post a Comment