Rais wa
Tanzania Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kuzindua rasmi shughuli za bunge
la kitaifa kuhusu marekebisho ya katiba mjini Dodoma katika hatua
itakayoanzisha rasmi mjadala wa kitaifa kuhusu marekebisho hayo.
Bunge
hilo maalum la katiba limepewa kati ya siku 70 hadi 90 kujadili rasimu
ya katiba na kisha kuifanyia marekebisho kabla ya kura ya maamuzi.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya wajumbe kutoka upinzani na mashirika ya kiraia yanapanga kuvuruga shughuli hiyo ya uzinduzi.
Suala la
hotuba ya Rais Kikwete limekuwa sehemu ya mjadala katika Bunge hilo
kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha
Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge kwa mujibu wa kanuni.
Mjadala
huo uliwafanya baadhi ya wajumbe kumzuia Jaji Warioba Jumatatu iliyopita
kuwasilisha rasimu hiyo kama ilivyokuwa imepangwa.
Kikao cha
maridhiano kilifanyika siku hiyohiyo usiku na kufikia mwafaka kwamba
Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe Rasimu
ndiposa Rais aweze kuzindua shughuli ya kujadili rasimu hiyo kabla ya
kura ya maoni.
CHANZO BBC SWAHILI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment