Oprah Winfrey na Howard Schultz
Oprah ameungana na rafiki yake bilionea Howard Schultz wa kampuni ya Starbucks katika kuanzisha mradi huo wa majani ya chai, ambao umetangazwa Jumatano ya wiki hii wakati wa mkutano wa kila mwaka wa kampuni hiyo.
Majani hayo ya ‘Oprah Chai’ yatapatikana katika ladha mbalimbali ikiwemo ya mdalasini, tangawizi, iliki pamoja na karafuu.
Katika kila bidhaa ya ‘Oprah Chai’ itakayouzwa, kampuni iliyoingia ubia na Oprah ya Starbucks itatoa mchango kwa shule ya wasichana iitwayo ‘Oprah Winfrey Leadership Academy’ iliyoianzishwa na inayofadhiliwa na Oprah, iliyoko nchini Afrika Kusini.
Oprah Chai itaingia sokoni (April 29) huko Marekani na Canada.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment