Akiwa amevua shati huku akiwa anaombewa. |
Vitenda kazi vyake vikiwa vimemwagwa chini. |
Kazi kwelikweli. |
Alikosea njia meeen, akakutana na Yesu meen. Picha kwa hisani ya Ufufuo Crew. |
Katika hali
isiyo ya kawaida mtu huyu ajulikanaye kwa jina la Shabani Hamis amenaswa
akiwa anafanya uchawi katika kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.
Matukio ya kunaswa wachawi yamekuwa mengi kanisani hapo kutokana na
uweza wa Mungu unaojidhihirisha kupitia Mchungaji Kiongozi wa kanisa
hilo, Frank Andrew.
Pamoja, na kukutwa bila nguo mtu huyo aliyekuwa amebeba vifaa ambavyo
kwa mujibu wa maelezo yake, huvitumia kuwanga na kupaa ni pamoja na
tunguli na kikapo cha mkoba wa uchawi. Tukio hilo la aina yake limetokea
Usiku wa saa sita, wakati mkesha wa maombi ukiendelea kanisani hapo.
Baada ya maombi makali ya kuharibu uchawi katika anga la Arusha,
ikafuatiwa na tukio hilo. Mungu ni mkuuu maana hapana uchawi wala Uganga
juu ya watu wa Mungu.
Information Ministry - Arusha
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment