.
Wizara ya
mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini ambayo
yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa, wazazi
kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.
Majina
hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye maana
Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu
linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini.
Mengine
katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu yanaaminika kuwa
yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au yenye kupingana
na tamaduni na dini ya falme hiyo.
Sababu
nyingine ni ya kigeni ama ya ughaibuni yakiwemo yenye maana ya ufalme au
ukubwa, cheo flani kama Sumuw (mtukufu), Malek (mfalme) na Malika
(Malkia).
Majina
mengine hayapo katika jamii hizi hivyo hakuna sababu zilizotolewa juu
yake, hii ni sehemu nyingine ya orodha yenyewe ambapo ni Malaak (angel),
Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Arabic for Benjamin)
Naris, Yara, Sitav.
Maya
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment