KOMPYUTA
zinazotumia windows XP hazitoweza kupokea taarifa muhimu na kuongezeka
mashambulizi ya virusi vya spyware vinavyoharibu taarifa binafsi na
takwimu za kibiashara baada ya mwezi mmoja. Hayo yamebainishwa jana na
Mkurugenzi wa Microsoft kwa kanda za Afrika Mashariki, Magharibi,
Rotimi Olimide.
Alisema
kuwa utafiti mpya wa Microsoft umeonyesha kuwa Window XP hushambuliwa
kirahisi na virusi mara tano zaidi huku usalama wake ukiwa mdogo kiasi
cha kuruhusu wizi wa mtandao.
Alisema
ni vyema ndani ya mwezi mmoja, watumiaji wa window hiyo wakabadilika na
kuhamia Window 8 ambayo ina uwezo mkubwa wa kuhimili mshambulizi ya
virusi.
“Mfumo uliotengenezwa kwenye Window XP ni wa kizamani na uendeshaji wake sio iliyoundwa kujilinda dhidi ya virusi.
“Baada
ya mwezi mmoja si kuwa huduma ya Window XP haitafanya kazi, unaweza
kuendelea nayo lakini usalama na utendaji wake hautakuwa mzuri ,”
alisema.
Alisema
mfumo wa uendeshaji wa Windows 8 na Office 365 unatoa ulinzi wa uhakika
na ufanisi. Mkurungezi wa Teknolojia na Uendeshaji, Chege Thumbi
alisema ni vyema hasa taasisi za kifedha kuacha kutumia windows XP mara
moja ili kuwa katika usalama na urahisi wa kufanya biashara.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment