Asilimia 95.5 ya wapiga kura wanaunga mkono Crimea ijitenge kutoka kwa Ukraine na kujiunga na Urusi.
Maafisa waliosimamia kura hiyo ya maoni amesema kuwa baada ya kuhesabu takriban nusu ya kura zilizopigwa .
Kiongozi wa jimbo hilo amesema kuwa atatuma rasmi ombi la kutaka kujiunga na urusi hapo kesho .
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa ataheshimu uamuzi wa wapiga kura.
Marekani na
Jumuiya ya Ulaya wametaja kura hiyo ya Maoni kuwa ni haramu na wamesema
kuwa hawatatambua matokeo yake kwani ilipigwa katika ''hali ya vitisho
vya kupigwa'' vilivyotolewa na wanajeshi wa Urusi.
Siku
ilikamilika kwa amani katika rasi hiyo, ingawa kulikuwa na maandamano
katika katika miji iliyoko Mashariki mwa Ukraine, kukiwemo mapigano
mengine katika Doneski.
Watu wanaounga mkono Urusi walichukua utawala wa jimbo hilo la Crimea tangu mwezi Februari.
Chanzo: Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment