Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

WAKATI masuala ya ushoga yakipingwa kwa nguvu zote hapa nchini, skendo ya aina yake imeikumba serikali baada ya siri kuvuja kuwa mmoja wa viongozi kumi wa juu nchini ni shoga.

Taric Jumbe akitoa ushuhuda jinsi alivyofanya mapenzi na kigogo huyo.
Habari hizo za kushtua na kufedhehesha taifa ambazo zimefanyiwa kazi na paparazi, zilitua hivi karibuni chumba cha habari kupitia kwa kijana aliyejitokeza na kueleza alivyofanya mapenzi ya jinsia moja na kigogo huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa.
KIJANA HUYO NI NANI?
“Mimi naitwa Taric Jumbe, nina miaka 21, nimefika hapa kutoa ushuhuda wangu kuwa nilifanya mapenzi na... (anataja jina), tulianza kuchat kwenye Facebook, akaniomba urafiki, nikamkubalia nikijua ni wa kawaida tu.
“Baadaye akaanza kunitongoza na kuniahidi fedha nyingi, nikakubali. Siku ya kwanza tulikutana Dar, Hoteli ya Serena, akanielekeza chumba alichopo (anataja namba ya chumba), nikaenda na kuwakuta walinzi wake, nilipojitambulisha wakaniruhusu kuingia chumbani kwake. Nimeshafanya naye mara tatu,” alisema kijana huyo.

JINSI WALIVYOWASILIANA
Mbali na matumizi ya mtandao wa kijamii, wanahabari wetu walitaka kujua mpaka kijana huyo anafika hotelini hapo, alikuwa akiwasiliana na kigogo huyo kwa njia gani? Jumbe akasema:
“Mwanzo nilikuwa nawasiliana naye kwa Facebook lakini tulipozoeana alinipatia namba zake za simu.”
 
Jibu hilo lilitoa mwanya kwa makachero wa gazeti hili kuperuzi mtandao wa simu ile ili kujua kama anayeitumia namba hiyo ni kigogo huyo au ni changa la macho.
Bila chenga ilibainika kuwa namba hiyo ni ya kigogo huyo, lakini ilipopigwa kwa lengo la kuwasiliana naye moja kwa moja, iliita bila kupokelewa na kuwafanya waandishi kuendelea na kazi ya kumhoji kijana huyo kwa kina.
Taric akiwa ndani ya Global kuelezea sakata hilo la kufanya mapenzi na kigogo serikalini.
KUHUSU MALIPO
Jumbe aliweka wazi kuwa siku ya kwanza kukutana naye alilipwa shilingi elfu themanini sambamba na ahadi kuwa wakati wowote atakapokuwa na shida awasiliane na kigogo huyo ambaye msafara wake huongozwa na pikipiki yenye king’ora na gari la polisi, kwa lengo la kuwezeshwa kimaisha.
Aliongeza kuwa kiasi kikubwa alichowahi kuhongwa ni shilingi laki tatu (300,000), huku akiainisha kwamba fedha nyingine alikuwa akipewa kidogokidogo kwa ajili ya kujikimu.
MSHANGAO MWINGINE
Mbali na kijana huyo kukiri kufanya mapenzi mara mbili na kigogo huyo hotelini, mshangao ulikuja pale alipoweka wazi kuwa mara ya tatu alimfuata kiongozi huyo nyumbani kwake ambako alishirikiana naye tendo hilo la aibu.
Waandishi walipotaka kujua waliwezaje kufanya uchafu huo nyumbani kwa kigogo huyo mwenye familia, Jumbe alisema: “Ni kweli anaishi na familia lakini nje ya nyumba yake ana ofisi, huko ndiko alikonikaribisha na kunifanyia mchezo huo.”
 
UPEKUZI WA MAWASILIANO
Baada ya maelezo hayo, waandishi wetu wa paparazi waligeukia uchunguzi wa mawasiliano ya simu na mtandao wa Facebook baina ya Jumbe na kigogo huyo ambapo walibaini kuwepo kwa mambo ya aibu kubwa.
 
Kwa macho maangavu, waandishi wetu walioneshwa meseji alizokuwa akituma kigogo huyo ambazo chache kati ya hizo zilisomeka: “Baby, mke wangu, honey,” huku Jumbe naye akichagiza majibu kwa mtindo huohuo hadi naye kufikia mahali pa kumwita kigogo huyo ‘mume wangu’, aibu iliyoje!
Kama hiyo haitoshi, wawili hao walifikia hatua ya kusifiana namna walivyoumbika na kupeana mapenzi motomoto na kuahidiana kuwa pamoja milele. Kufuru kubwa kwa Muumba!
 
WIVU HAUKUKOSEKANA
Katika hali ya kustaajabisha na kuonesha kuwa kigogo huyo amekubuhu kwenye mambo hayo, wakati mwingine akiwa nje ya nchi alidiriki kumuonea wivu kijana huyo ambapo mara kadhaa alituma meseji ya kutishia kumwacha kutokana na kile alichokiita ‘kutoka nje ya ndoa’.
Moja kati ya meseji hizo za fedheha kutoka kwa mheshimiwa huyo, ilimtuhumu Jumbe kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine, jambo ambalo kijana huyo alilikanusha na wote kuwekana sawa kwa lengo la kusonga mbele na uhusiano wao.
KIGOGO MZITO AHOJIWA
Baada ya kupata maelezo hayo ya kutisha na kusikitisha, kwa zaidi ya mwezi mzima, paparazi ilifanya juhudi za kumtafuta kigogo huyo ili kuweza kupata maelezo yake kuhusiana na mkaspaparazi iliweza kumfikia na kummwagia data zote, zikiwemo picha za kijana huyo na nakala ya mawasiliano katika mtandao wa Facebook ambapo alionekana kuduwaa.
Hata hivyo, kutokana na waandishi wetu kufanya mahojiano na kigogo huyo huku wapambe wake wanaomlinda na kumuongoza wakiwepo, haikuwezekana kufungua kila kitu wazi kwa vile mazungumzo hayo yalikuwa yakirekodiwa.
Baada ya kuoneshwa tuhuma zake kwa kutumia nyaraka, mheshimiwa huyo alikiri: “Nazifahamu hizi nyaraka.” Akimaanisha alichokiona kinamhusu kwa asilimia mia moja.
 
TAHADHARI
Tunapenda kuutaarifu umma kuwa tumeamua kulificha kwa makusudi jina la kigogo huyu ili kuilinda heshima yake ambayo ni kubwa katika jamii yetu. Tutaliweka wazi wakati wowote endapo kati ya mambo haya yatajitokeza.
 
Mosi, kijana huyo (Jumbe) atadhuriwa. Tunajua nguvu alizonazo mheshimiwa huyu ni kubwa, tunaomba kumfahamisha kwamba tutamuanika hadharani endapo Jumbe atafikwa na matatizo yoyote yasiyo ya kawaida.
 
Pili, endapo tutathibitisha kuwa anaendelea na mchezo wake huu usiokubalika na mwisho, endapo waandishi waliokwenda kufanya naye mahojiano, ambao yeye na wapambe wake wanawafahamu, watapata madhara yoyote

credit:GPL

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top