MADEREVA
wa daladala Manispaa ya Morogoro wamegoma asubuhi hii wakidai kukamatwa
hovyo na matrafiki na hakuna daladala linalofanya safari yoyote katika
manispaa hiyo.
Madereva hao wanadai wameamua kugoma kutokana na kamatakamata ya
askari wa usalama barabarani, ambapo wamesema daladala moja kwa siku
linaweza kukamatwa hadi mara nne na wakihoji wanaambiwa ni makosa
tofauti.
Waliongeza kuwa wamepeleka malalamiko yao ngazi mbalimbali za serikali mkoani Morogoro bila mafanikio.
Mgomo huo umewaathiri zaidi wanafunzi ambao wapo katika mitihani
ya nusu muhula ambapo baadhi yao walilazimika kutembea kwa miguu huku
wengine wakirudi nyumbani kujipanga.
Ili kuongeza uzito katika mgomo huo, madereva hao wametoa
tahadhari kwa wamiliki wa mabasi ya Abood kutojaribu kupeleka mabasi yao
barabarani kama ambavyo wamekuwa wakifanya pindi ukitokea mgomo ndani
ya manispaa hiyo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment