Wakizungumza wa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea
Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki
wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa kulipa
pesa ndogo wanapowaopoa.
“Yaani sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa
vizuri tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata
mjumbe wa bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako!
Wanalipa vizuri ile mbaya.
“Kipindi cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au
20,000 lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo,
tusipojenga safari hii basi tena,” alisema msichana mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha
biashara ni eneo Chako ni Chako.
Mwingine ambaye aliomba jina lake lisiandikwe mtandaoni akidai yuko
Dodoma bila ndugu zake walioko Dar kujua alisema: “Unajua hii biashara
inakuwaga na usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini
sasa hivi wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba
ndogo zao kabisa.”
Hata hivyo, uchunguzi wa paparazi umebaini kuwa, biashara hiyo sasa
imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho zao za
siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao.
paparazi alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni Chako,
Mwenga Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na Maisha
na kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha kuondoka.
paparazi inatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya walichokifuata
bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale wasichana
walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza, wajue
kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.
credit:GPL
Post a Comment
Post a Comment