Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


MWANAMUZIKI kutoka Marekani Chris Brown, ambaye hivi sasa ametupwa rumande anadaiwa kuwa ataruhusiwa kuoga mara moja tu ndani ya siku mbili akiwa jela.

Mwanamuziki huyo wa miondoko ya R&B, alitupwa jela wiki hii ambako atakaa kwa mwezi mzima baada ya kufukuzwa rehab.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umedai kuwa Brown atafungiwa kwenye chumba chake pekee yake kwa zaidi ya masaa 23 kila siku, ingawa ataruhusiwa kusoma vitabu pamoja na kufanya mazoezi.
Ambapo atakaa jera hadi 23 April, ambapo ametolewa Rehab baada ya kufanya vitendo vinavyoenda kinyume na sheria ya rehab ikiwa moja wapo kumshika mwanamke kinyume na masharti ya huko.

Brown ameponzwa na tabia yake ambapo, alimshika mwanamke kinyume na masharti ya humo pamoja na kukaataa kuchukua vipimo vya dawa ya kulevya na kwa kutoa kauli za vitisho wakati wa 'therapy' ya kundi kwa kudaiwa kusema kuwa 'i am good at using guns and knives'.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top