Na Mwandishi wetu,Geita yetu Blog
WIKI moja baada ya Tanzania kuungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha siku ya wanawake duniani,kauli mbiu ikiwa ni "chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia" mkoani Geita hali imekuwa tofauti baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Modester Shija (55-60) mkazi wa kitongoji cha Kamlale,kijiji cha Nyawilimilwa kata ya Kagu wilayani hapa kuuliwa kikatili kwa kukatwa mapanga Machi 14,mwaka huu na watu wasiojulikana.

Imeelezwa
kuwa Machi 14,majira ya saa 19:30 jioni Bi.Modester Shija akiwa jikoni
anaandaa chakula cha usiku walifika wanaume wawili waliovalia makoti
meusi mara baaada ya kukaribishwa mmoja wa wanaume hao aliomba maji ya
kunywa mara baada ya kunywa maji aliingia jikoni alikokuwa mama huyo
huku akisikika anauliza kwa kisukuma "mayo otale kubiisha? akimaanisha
Hujaivisha? kabla ya kujibiwa ilisikika sauti ya kulalamika ya mwanamke "
nimewakosea nini? wakati kijana mmoja anakwenda kuangalia ni kitu gani
kinatokea nao naye akatishiwa panga ndipo akakimbia huku akipiga kelele
za kuomba msaada.
Akizungumzia
tukio hilo la kusikitisha mmoja wa watoto wa marehemu Juma Chalula (23)
alidai kuwa siku ya tukio majira ya saa moja na nusu jioni wakati
anajiandaa kwenda kuoga baada ya kutoka shambani,walifika wageni wanaume
wawili ambao hawatambui mara baada ya kuwakaribisha nje mmoja aliomba
maji ya kunywa,alimfuatia jikoni,baada ya kumaliza kunywa maji alisema
ngoja awasalimie jikoni,baada ya muda kidogo alisikia mama yake akipiga
kelele wakati anaenda kumsaidia akathibitiwa na yule aliyekuwa amebaki
nje baada ya kuchomoa panga.
"wale
watu walivalia makoti meusi kumbe ndani walificha mapanga,mmoja
aliniomba maji ya kunywa baada ya kumaliza akadai asalimie jikoni kumbe
alikuwa anakwenda kumuua mama yangu,dakika aikuisha nikasikia mama
anasema kwa sauti ya kulalamika akidai" nimewakosea nini jamani" wakati
naenda kuangalia nikatishiwa na kukimbizwa na mmoja aliyekuwa amebaki
nje,nilikimbia huku napiga yowe ila sikupata msaada wa haraka kutokana
na nyumba zetu kuwa mbalimbali" alisimulia Juma Chalula mtoto wa
marehemu
"siku
hiyo nilisikia saa moja jioni "mwamo" yaani yowe ila baada ya kufika
kwenye tukio tulikuta wameshaondoka hao wauaji,kiukweli kwenye kitongoji
changu ni tukio la kwanza na limetushtua sana,na kwa hali hii lazima
tuwasake hao watu na tuwapate" alisema Mwenyekiti wa kitongoji.
Mwenyekiti
wa kitongoji hicho Bw.Mashauri Elisha alidai kuwa baada ya kusikia yowe
aliwaongoza wananchi kuellekea eneo la tukio amba baada ya kufika
walikuta tayari mama huyo akiwa ameuliwa kwa kukatwa panga shingoni na
kwenye mabega yake huku mwili wake ukiwa umelala jikoni ndipo walipoanza
kuwasaka wauaji hao ila hawakuwapata.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Nyawilimilwa Bw.Charles Kumalija alidai kuwa atahakikisha anasaidiana na polisi ili wauaji hao wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo husika,aliwataka wananchi kuwafichua waalifu wote ili sheria ichukue mkondo wake dhidi yao.
"yeyote anayefahamu hawa watu wanaojihusisha na vitendo hivi viovu alete taarifa ili wakamatwe la sivyo watatumaliza,haya matendo yanatutia aibu ni mambo ya kizamani tunatakiwa kubadilika" alisema Kumalija
Jeshi la polisi wilayani Geita limethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kudai chanzo bado kinachunguzwa na kwamba linamshikilia Hamis Chalula (41)mkazi wa Kamlale kuhusiana na tukio hilo

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment