Home
Β»
Matukio
Β» Ofisa Elimu Atiwa Mbaroni Katavi Akituhumiwa Kumchoma Kisu Na Kumuua Mgoni Wake Aliyemfumania Akifanya Mapenzi Na Mkewe
Polisi mkoani Katavi inamshikilia Mratibu Elimu Kata ya Katuma wilayani Mpanda, Mohamed Muna (59) kwa tuhuma za kumchoma kisu na kumuua mkazi wa kitongoji cha Misheni, Gidison Vincent (32), anayedaiwa kuwa mgoni wake.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alimuua Gidison baada ya kumfumania ndani ya nyumba yake akifanya mapenzi na mkewe, Ester Kasansa βChukiβ (36).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari akithibitisha alisema mkasa huo ulitokea Januari 27, mwaka huu saa 02:30 usiku, katika Kitongoji cha Mashineni, Kata ya Katuma wilayani Mpanda.
βUsiku huo wa tukio, mtuhumiwa alimkuta Gidison (sasa marehemu) akiwa ndani ya nyumba yake akifanya mapenzi na mke wake aitwaye Ester, ndipo alipogonga mlango wa chumbani na mgoni wake (marehemu) kutoka nje na kuanza kupambana naye, ambapo mtuhumiwa alimchoma kisu kifuani na kukimbia,β Kidavashari alisema.
Kwa mujibu wa Kidavashari, chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika ili kujibu tuhuma inayomkabili.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment