Home
Β»
Kitaifa
Β» Mahakama Ya Rufaa Kuamua Ugomvi Wa Nyumba Kati Ya Afande Suleiman Kova Na Godfrey Nzowa
Mahakama ya Rufaa wiki ijayo inaanza kusikiliza kesi za rufani 50 za jinai na madai katika Kanda ya Arusha ikiwamo rufaa ya makamishna wawili wa Jeshi wa Polisi wanaogombea nyumba ya serikali iliyopo Uzunguni Arusha.
Maofisa hao, Godfrey Nzowa ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya katika Jeshi hilo amemshitaki mahakamani aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akipinga kuuziwa nyumba hiyo. Kamishna Kova hata hivyo amestaafu rasmi mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa orodha ya kesi zitakazosikilizwa na majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa kwa mwezi mmoja mjini hapa, Nzowa anamlalamikia Kova na wenzake kupinga kuuziwa nyumba hiyo aliyokuwa akiishi alipokuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Arusha.
Nyumba hiyo aliuziwa Kamishna Kova akiwa ameshahama mkoani Arusha na wakati inauzwa Nzowa alikuwa akiishi katika nyumba hiyo, familia yake akiwa RCO kabla ya kuhamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuendelea na wadhifa huo, Kova akiwa bosi wake.
Orodha hiyo yenye jumla ya mashauri 50 inaonesha mahakama hiyo itasikiliza rufani ya Wakili maarufu jijini Arusha, Median Mwale ambaye amekata rufaa dhidi ya Jamhuri katika kesi yake ya kudaiwa kutakatisha fedha chafu na kujipatia mabilioni ya fedha kwa njia ya udanganyifu akiwa na wenzake watatu.
Rufani hiyo namba 395 ya mwaka 2013 ya Wakili Mwale dhidi ya Jamhuri imepangwa kusikilizwa na majaji watatu, Mbarouk Salim Mbarouk, Bernard Luanda na Semistocles Kaijage watakaosikiliza pia mashauri mengine kabla ya kutoa uamuzi Machi 5, mwaka huu.
Orodha iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, E.Y. Mkwizu inaonesha kesi nyingine yenye mvuto ni ile ya wafanyabiashara Philemon Mangβehe na Gesso Bajuta iliyodumu kwa miaka 20 sasa.
Katika kesi hiyo, Mangβehe wa Kampuni ya Bukine anamdai fidia ya mamilioni ya fedha Bajuta baada ya kudai kuharibiwa biashara yake ya kusambaza vifaa vya ofisi katika Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) mwaka 1996.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 9 201609 Sep 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September 09 201...Read more ?
- Viongozi wa Afrika Mashariki Waigomea Ulaya....Wajipa Miezi Mitatu Kuutafakari Mkataba wa EPA09 Sep 20160
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa miezi mitatu kuju...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Majibu ya Waziri mkuu Majaliwa Leo Bungeni kuhusu wahusika wa mauaji ya askari08 Sep 20160
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na ...Read more ?
- Makamu wa Rais: Viongozi Na Watumishi Wa Umma Kuchukuliwa Hatua Kali Iwapo Watabainika Kukiuka Taratibu Za Kazi08 Sep 20160
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya M...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment