Home
Β»
general news
Β» Serikali Kutoa Bei Ekezi Uuzaji Ardhi Ili Kuwawezesha Wananchi Wasio Na Uwezo Kiuchumi
SERIKALI inatarajia kutoa bei elekezi ya uuzaji wa ardhi, tofauti na hali ya sasa ambayo viwanja vimekuwa vikiuzwa kwa bei ya juu na kufanya watu wasio na uwezo kiuchumi kushindwa kumiliki na kujenga nyumba.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi alisema jana kwamba serikali inaandaa utaratibu wa kutoa bei hiyo elekezi, itakayohusu watu wote.
Alitoa taarifa hiyo jana mjini Kibaha katika mkoa wa Pwani, wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kutaka kufahamu kero mbalimbali zilizo kwenye Idara ya Ardhi katika mkoa wa Pwani, zinazokabili wananchi.
Alisema bei dira hiyo itakuwa kwa watu wote wanaouza ardhi kwa maana kwamba, kabla ya kuuza, watatakiwa kuwasiliana na serikali ili wananchi wapunguziwe kero ya kushindwa kumiliki ardhi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo. Alisema ardhi ni huduma na si biashara.
Waziri Lukuvi alisema baadhi ya watu wamefanya ardhi, kama ndiyo sehemu ya kujinufaisha kwa kununua mashamba, kisha kuyagawa viwanja ambavyo huviuza kwa bei kubwa. Alisema jambo hilo limekuwa likisababisha wananchi wa kawaida, kushindwa kumudu kununua viwanja.
βMsifanye ardhi kama biashara. Hii ni huduma na huduma haipaswi kutozwa gharama kubwa. Utashangaa eneo kama Kibaha, kiwanja kinauzwa kiasi cha shilingi milioni kumi. Kwa mtu wa hapa ana uwezo gani?β alisema.
Aliendelea kusema, βKwa mfano, pale Kibada viwanja vilikuwa vikiuzwa kwa shilingi milioni tatu tu hatuwezi kukubali hali hii iendelee.β
Alisema hata wale ambao wamewekeza ardhi kwa muda mrefu na kufanya kama rehani kwa ajili ya kukopa fedha kwenye benki zao, wamekuwa ni tatizo kubwa.
Alieleza kwamba, wengi wao wanaoomba mashamba makubwa serikalini, wamekuwa wakibadili mashamba hayo na kuwa viwanja ambavyo huviuza kwa bei mbaya. βNa ni hao hao wanamiliki maeneo mbalimbali hapa nchini kwani majina ni yale yale,β alisema.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Jamaa Aliyejitosa Zoo Aliwe na Simba Laivu Alikuwa Anadai Mwisho wa Dunia Umefika...23 May 20160
Inasikitisha kwakweli, ameokolewa.... na simba walioanza kumla waliuwawa. aliingia kwenye jumba ...Read more ?
- Watumishi HEWA Waziponza Benki.......Benki za Dar es Salaam Zalimwa Barua Kurejesha Mamilioni ya Shilingi23 May 20160
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa zikitumika kuwek...Read more ?
- Waziri Nchemba Afanya Ziara Ya Kushtukiza Saa Saba Usiku Machinjio Ya Ukonga Mazizi Na Kufukuza Viongozi Wote Wa Machinjio12 Feb 20160
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usiku...Read more ?
- Askofu Gwajima, Sheikh Wa Mkoa Dar Wakwama Kumjulia Hali Mufti12 Feb 20160
Jopo la Madaktari wanaomtibu Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir wamezuia ...Read more ?
- Siku 100 za Rais Magufuli: Hospitali Ya Muhimbili Yang'aa, Mapato Yapaa na Upatikanaji wa Dawa Waongezeka Kwa Asilimi 9611 Feb 20160
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam imesema ndani ya siku 100 z...Read more ?
- Lowassa Atakiwa Kuvisaidia Vyombo Vya Dola Kukabiliana na Tishio La Kundi la al Qaeda Kuingia Nchini10 Feb 20160
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed amemtaka Wa...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment