Muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia Uchaguzi uliofutwa kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametangaza kuwa uchaguzi huo lazima urudiwe.
Wakizungumza jana na vijana wa chama cha Mapinduzi katika viwanja vya Maisara waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya matembezi ya kuunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar,viongozi wa juu wa chama hicho walisisitiza kuwa uchaguzi wa Zanzibar upo pale pale na utarudiwa kadiri tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itakavyotangaza.
Wa kwanza kutoa msimamo huo alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, aliyesema kuwa uchaguzi huo utarudiwa hata ikiwezekana vyama vyote vikijitoa CCM kitashiriki peke yake
βUchaguzi wa marudio upo pale pale, tunajua uchaguzi ulifutwa kihalali, mjitayarishe kwa uchaguzi wa marudio. CUF wamesema watatumia nguvu ya umma, tunawakaribisha na wataona matokeo yakeβ alisema Balozi Iddi.
Katika mkutano huo uliokuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ZBC, Dk Alli Mohamed Shein alipongeza msimamo wa Balozi Iddi, na kusema atabaki kuwa rais hadi uchaguzi utakaporudiwa.
Dk Shein alisema yupo madarakani kwa kushauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwamba hajavunja katiba na kama itatokea mahakama ikatoa ufafanuzi kuwa anakosea kuwepo hapo kikatiba basi ataondoka madarakani
βMahakama ikisema nakosea nitaondoka, Rais yupo Baraza la Mapinduzi lipo na Mawaziri wapo, nitaita waandishi wa habari Ikulu na mimi nimjibu Maalim Seif kwani kuna mengi amenisingiziaβ alisema.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Jamaa Aliyejitosa Zoo Aliwe na Simba Laivu Alikuwa Anadai Mwisho wa Dunia Umefika...23 May 20160
Inasikitisha kwakweli, ameokolewa.... na simba walioanza kumla waliuwawa. aliingia kwenye jumba ...Read more ?
- Watumishi HEWA Waziponza Benki.......Benki za Dar es Salaam Zalimwa Barua Kurejesha Mamilioni ya Shilingi23 May 20160
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa zikitumika kuwek...Read more ?
- Waziri Nchemba Afanya Ziara Ya Kushtukiza Saa Saba Usiku Machinjio Ya Ukonga Mazizi Na Kufukuza Viongozi Wote Wa Machinjio12 Feb 20160
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usiku...Read more ?
- Askofu Gwajima, Sheikh Wa Mkoa Dar Wakwama Kumjulia Hali Mufti12 Feb 20160
Jopo la Madaktari wanaomtibu Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir wamezuia ...Read more ?
- Siku 100 za Rais Magufuli: Hospitali Ya Muhimbili Yang'aa, Mapato Yapaa na Upatikanaji wa Dawa Waongezeka Kwa Asilimi 9611 Feb 20160
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam imesema ndani ya siku 100 z...Read more ?
- Lowassa Atakiwa Kuvisaidia Vyombo Vya Dola Kukabiliana na Tishio La Kundi la al Qaeda Kuingia Nchini10 Feb 20160
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed amemtaka Wa...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment