Home
»
ACT -Wazalendo
»
SIASA
» Msani Maarufu wa Filamu Ajiunga na Chaa cha ACT- Wazalendo.......Wagombea Urais Kupitia Chama Hicho Kutangazwa Agosti 13
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari jana alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.
Akizungumzia mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, Mtemelwa alisema Julai mosi mwaka huu Chama Cha ACT-Wazalendo kilifungua rasmi pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali zikiweno za Udiwani, Ubunge na Urais.
Alisema tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kuchukua fomu na hadi sasa kuna baadhi ya majimbo na kata zina watia azma kuanzia wanne mpaka tisa jambo ambalo alidai ni faraja kwa ACT Wazalendo.
"Kati ya majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo tumeshakuwa na waweka azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima na tunaamini mpaka kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote 265 yatakuwa yanawatia azma mbalimbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu," alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo.
Alibainisha kuwa kichama mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi ya udiwani ni julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho ni Julai 31 na kwa nafasi ya Urais mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti Mosi, 2015.
"Kwa ngazi ya Taifa Halmashauri kuu itakutana Agosti 13 kwa ajili ya kuteua jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu.
"Agosti 13, Mkutano mkuu utamchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama cha ACT Wazalendo katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Hivi karibuni tumepokea taarifa kutoka katika miji ya Tarime na Rorya Mkoani Mara kuwa kuna watu wanapita na kutangaza kuwa Chama chetu kimezuiwa kushiriki Uchaguzi kwa muda wa miezi sita.
"Tumebaini lengo la upotoshaji huu ni kuwakatisha watanzania tamaa juu ya ukuaji wa Chama Cha ACT-Wazalendo pamoja na dhamira yake nzuri ya kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere.
"Tunawataarifu wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama hakitakuwa tayari kuona sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita bila kupingwa," alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa08 Sep 20160
Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kuhamia chama choch...Read more ?
- Msajili amlima Barua Maalim Seif kuhusu sakata la Lipumba01 Sep 20160
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananch...Read more ?
- Breaking News: Mbowe Atangaza Kuahirisha Maandamano ya Oparesheni UKUTA Yaliyokuwa Yamepangwa Kufanyika Kesho31 Aug 20160
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Opare...Read more ?
- Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana25 Aug 20160
Leo(Jana) nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tu...Read more ?
- Prof Lipumba:Sihusiki na Vurugu zilizotokea Katika Mkutano wa CUF23 Aug 20160
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ...Read more ?
- Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi23 Aug 20160
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Maha...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment