Steve aliitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) nakuwahimiza vijana wa Kinondoni wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu ili waweze kuchagua viongozi watakaoweza kuifikisha Kinondoni sehemu wanayotaka.
Katika mkutano huo, Steve alisindikizwa na wasanii mbalimbali akiwemo JB, Wasta, Bi Mwenda, Chuchu Hans, Johari,Ray Nyamayao, Esha Buheti, Thea na Bi Star
“Kinondoni tunaweza kuondokana na mafuriko kama tutachagua kiongozi atakayeweza kurekebisha miundombinu ya wilaya yetu”alieleza Steve huku akishangiliwa.
Mtanzania
Post a Comment
Post a Comment