WATU sita wamekufa na wengine 45 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea juzi na jana mkoani Singida.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema mjini hapa jana kuwa ajali ya kwanza ilitokea Juni 11 mwaka huu saa 1.30 usiku eneo la Manga nje kidogo ya mji huu kwenye Barabara Kuu ya Singida – Mwanza.
Alisema ajali hiyo ililihusisha basi lenye usajili wa namba T174 CAV Scania la Kampuni ya Nice Line linalomilikiwa na Enock Mwita wa jijini Mwanza ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza.
Dereva wa basi hilo aliligonga kwa nyuma gari la mizigo lenye namba za usajili RAT 317N/ RL 0754 aina ya Benz lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara hiyo na kusababisha vifo vya abiria watatu papo hapo. Wengine wawili walifia hospitalini na kusababisha majeruhi 37.
Kwa mujibu wa Kamanda Sedoyeka, dereva huyo ambaye alikimbilia kusikojulikana baada ya ajali kutokea, alikuwa kwenye mwendo kasi. Katika ajali nyingine iliyotokea Juni 12 saa 12.15 asubuhi katika eneo la Kindai kwenye barabara kuu ya Singida – Dodoma nje kidogo ya mji huu, gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 998 CWG liliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo cha abiria mmoja na majeruhi wanane.
Alisema abiria wa gari hilo walikuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuhudhuria mazikoi ya ndugu yao na gari lao lilipofika eneo la ajali kwenye kona kali dereva wake, Paul Bundala alishindwa kulimudu kutokana mwendo kasi.
Baadhi ya waliokufa katika ajali hiyo ni Shija Masanja,Yohana Chimole na Febronia Kway. Miili ya waliotajwa na wengine watatu ambao majina yao hayajatambuliwa imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida ambapo pia wamelazwa majeruhi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment